Friday, September 14, 2012

UMEWAHI KUSIKIA KWAMBA CHRIS BROWN ALIWAHI KUJIRUSHA KIMAPENZI NA AMBER ROSE? SOMA MAHUSIANO 15 YA MASTAA... YALIKUWEPO, HAYAKUWEPO?

1. Ray J na Whitney Houston (RIP)
Ripoti zilizagaa mwaka 2007, kwamba kaka yake Brandy alikuwa akitoka na (muimbaji marehemu sasa) Whitney Houston.

Hayo yaliyodaiwa kuwa mahusiano yao yalizua gumzo hasa kutokana na tofauti ya umri iliyokuwapo baina yao. Whitney alikuwa na umri wa zaidi ya miaka 20 ukilinganisha na wa muimbaji huyo wa R&B, Ray J.


2. Nas na Amy Winehouse (RIP)


Amy Winehouse na Nas walionekana mjini London mapema mwaka huu wakitoka kwenye sherehe ya kuzaliwa kwa Damian Marley.

Picha waliyopigwa ilizua utata hasa ikizingatiwa kwamba Winehouse alipata kurekodi wimbo ulioitwa "Me And Mr. Jones" ukidaiwa kuelezea mapenzi yake kwa rapa huyo, ambaye jina lake halidi ni Nasir bin Olu Dara Jones.


3. Gucci Mane na Mya                                                             
Gucci Mane na Mya walionekana katika klabu ya usiku ya Velvet Room ya mjini Atlanta mwaka 2009, katika pozi zilizoaminika kuwa za wapendanao.

Mya haraka alikanusha uvumi wa kuwa na mahusiano ya kimapenzi akisema:

    "Ule ulikuwa uvumi pia ambao ulinifanya nicheke. Hamna kuponda, ila kwa jinsi watu walivyogeuza mambo. Nilipiga picha naye kwenye klabu ile na meneja wangu alikuwapo. Nilitaka kumwambia kwaheri Gucci ndio maana nikasogea sikio mwake kumwambia kwa sababu sauti za muziki zilikuwa kubwa sana pale klabu, wakanipoga picha katika pozi ambalo sio sahihi ambalo lilinifanya nionekane nimemaliza kumbusu ama nilikuwa nambusu."

4. Amber Rose na Chris Brown
Uvumi ulizagaa kwamba Amber Rose na Chris Brown walijirusha kimapenzi mwaka 2009 baada ya pati ya Diddy, wakati bado akiwa na Kanye West.

Watu wengi walidai kuthibitisha uvumi huo kwa kutuma picha zilizoonyesha wawili hao wakila raha akiwamo rafiki mkubwa wa Chris Brown, Teyana Taylor ambaye alisema "walijiachia usiku kucha".
5. 50 Cent na Paris Hilton


50 na Paris Hilton walionekana katika pozi za kimahaba mjini Las Vegas mwaka 2007 kabla ya tamasha la tuzo za video bora za muziki za MTV Video Music Awards.


Kinara huyo wa kundi la alikanusha kujihusisha kimapenzi na mtoto huyo wa tajiri na baadaye akazua utata baada ya kumtimua stejini akimwambia "Get the f*ck off the stage" katika moja ya maonyesho yake, na kudaiwa kumfanya Paris aondoke akilia.

6. Ray J na Lil Kim
Ray J na Lil Kim
Katika kipindi kile kile ambacho Ray-J alionekana na Whitney Houston, muimbaji huyo wa R&B ambaye pia ni maarufu kwa "video ya chumbani" aliyoirekodi na mpenziwe wa zamani Kim Kardashian, alionekana tena akiwa na Lil Kim.

Ray J na Lil Kim ambao walifanya wimbo wa pamoja wa "Wait  Minute" walionaswa na picha za tovuti ya TMZ mwaka 2007 wakiwa wameshikana mkono kwa mkono.


Ray J akipozi na Lil Kim


7. Drake na Rihanna


Drake na Rihanna waliripotiwa kujiachia mwaka 2009 mjini New York.

Drake awali alikanusha ripoti kuhusu mahusiano yao, "Sio kweli kabisa. Mimi niko muwazi kabisa. Rihanna ni rafiki yangu, ni hivyo tu. Ni msanii mkubwa."

Kisha baadaye Drake akaanza kumwaga kidogo kidogo dondoo kuhusu mahusiano yao ya muda mfupi yaliyotokea usiku wa Mei.


Rihanna akitumbuiza na Drake


8. Kim Kardashian na Kanye 
HIVI SASA NI WAPENZI KWELI!Kulikuwa na ripoti mwaka 2010 kwamba sababu iliyofanya kuvunjika kwa mahusiano ya Kim Kardashian na boifrendi wake wa wakati huo Reggie Bush ilikuwa ni kimwana huyo kuiba mapenzi nje na rapa Kanye West.

Kardashian alikuja juu na kusema uvumi huo ulikuwa ni "uongo mtupu" lakini baadaye Kanye West akaonekana akimshika kimapenzi kimwana huyo wakati akirekodi kipindi chake cha televisheni cha "Keeping Up With The Kardashians" kwa mujibu wa jarida la Touch Magazine ambalo liliandika:

    "Kanye alikuwa ameuzungusha mkono wake kiunoni mwa Kim kwa jioni nzima! Alikuwa akipapasa goli lake (Kim) usiku kucha – walionekana kuwa wapenzi."


Picha ya wakati huo ya Kim Kardashian na Kanye West


9. Rihanna na Kanye West


Mwaka 2008 Jarida la Star liliripoti kwamba Rihanna na Kanye walionekana wakibusiana kimahaba nyuma ya jukwaa wakati wa onyesho la T.I..

    “Rihanna alikuwa amekaa kwenye mapaja ya Kanye, akiimba pamoja akifuatisha muziki. Muda mfupi baadaye wawili hao walikuwa wakibusiana kimahaba. Watu walistushwa. Baada ya muda, Rihanna lazima atakuwa alistukia kwamba watu walikuwa wanawaangalia, kwani aliwachukua walinzi wake wamsindikize kwenye chumba cha kuvalia."


10. Amber Rose and Reggie Bush


Mwaka 2010 uvumi ulizagaa kwamba Amber Rose aliachana na Kanye West na kutua kwa nyota wa mchezo wa American Football, Reggie Bush, ambaye alikuwa ni boifrendi wa zamani wa Kim Kardashian.

Amber Rose na Reggie Bush waliripotiwa kuonekana wakijiacha kimahaba.

Jarida la HollywoodLife liliripoti:

    "Mwanamitindo mwenye umri wa miaka 27, ambaye ameachana na rapa Kanye West mapema mwezi huu baada ya kudumu naye kwa miaka miwili, aliushika mkono wa Reggie, akamuangalia kimapenzi machoni na akaanza akaanza kudansi mbele yake. Ingawa kulikuwa kuna muziki unapigwa kwenye "background", Amber alikuwa akidansi kwa biti zake mwenyewe na Reggie alionekana kufurahia kila sekunde."

Reggie Bush na Amber Rose
11. Trina na Kobe


Mwaka 2009 kulikuwa na ripoti za ngumi baina ya rapa Trina na Vanessa, mke wa Kobe Bryant zilizotokana na mstari wa rapa huyo mwanadada uliosema,

    "Huyu nigga anadhani mimi nababaikia saa yake ya Rolex, unahitaji zaidi ya hilo kupita katikati ya mapaja yangu. Gari linaloruka, pengine nyumba iliyojengwa angani, najua unataka kupata haraka, wakati mimi ndiye mal*ya ambaye Kobe aliiba naye mapenzi nje ya ndoa yake…”

Trina baadaye akaendelea kukanusha kulala na Bryant na kutoa taarifa iliyosema mstari huo ulikuwa ni wa "kupikwa tu."

Trina


12. Wale na Solange
Wale na Solange Knowles


Mwaka 2009, rapa wa kibao cha DMV, Wale alitawala vichwa vya habari baada ya kubainisha mapenzi yake kwa mdogo wa Beyonce, Solange Knowles.

Wawili hao walifahamika kwa kuchombezana kwenye Twitter kabla ya kuanza kuonekana pamoja Central Park.

Kufuatia jambo hilo, Wale aliiambia Honey Magazine,

"Nampenda Solange, sisi ni marafiki. Ni binti mzuri. Mwanamke yeyote ambaye analea mwanae mwenyewe anachangia jamii kama yeye — ninawapenda sana."


Solange Knowles14. Khloe Kardashian And Jeezy
Khloe na Young Jeezy


Mwaka 2008 kulikuwa na ripoti kwamba binti mdogo zaidi wa familia ya akina Kim Kardashian, Khloe Kardashian anajiachia na rapa Young Jeezy.

Wawili hao walionekana wakijiachia katika pati ya mjini Vegas ya kusherehekea kutimiza umri wa miaka 24 ya kimwana huyo pamoja na Reggie Bush na Lauren London.
Khloe na Young Jeezy


14. Diddy na Sienna Miller
 Diddy na Sienna Miller


Muda mfupi baada ya watoto mapacha wa Diddy kuzaliwa, kulikuwa na ripoti kwamba alikuwa akijirusha na muigizaji Sienna Miller.

Kamera za tovuti ya TMZ ilimnasa Diddy akiingia katika chumba cha hoteli pamoja na Miller na alionyesha sura ya fadhaa alipoona anapigwa picha.
    Ripoti ya TMZ ilisema: “Diddy, baba wa mapacha wapya, alionekana akimshusha Miller katika hoteli yake ya NYC asubuhi hii baada ya kuripotiwa kuwa panoja naye usiku mjini hapa. Diddy alionyesha sura ya fadhaa wakati alipobaini kamera zinamnasa — na tumeambiwa kwamba alimtuma bodigadi kujaribu kushinikiza picha zilizopigwa zifutwe."


Diddy akiwa na Sienna Miller

15. Amber Rose na Fabolous
Amber Rose na Fabolous


Uvumi ulizagaa Oktoba kwamba rafiki wa kike wa zamani wa Kanye, Amber Rose alihamia kwa Fabolous na kwamba alikuwa na ujauzito wa rapa huyo.

Wote Amber na Fab walikanusha uvumi kwamba ni wapenzi na kwamba ana ujauzito.

Amber aliandika katika ukurasa wake wa Twitter akisema,

"Whoa…Lol mimi SI MJAMZITO…Tafadhali watu wa internet ni waongo kwa 97% KUHUSU MIMI…si msichana yule ambaye wanamtengeneza kuwa."

Fabolous pia alikanusha katika Twitter akisema,

    “Naona tovuti ya Media Takeout ndio CNN ya 'uswazi'.. Licha ya uvumi huu, mimi sijampa mimba mtu yeyote.. #ItAintMineTweet”

No comments:

Post a Comment