Saturday, September 1, 2012

BALOTELLI KUPASULIWA JICHO

Mario Balotelli (kushoto) akitoa uwanjani huku akielekezwa jambo na kocha Roberto Mancini

KOCHA wa Manchester City, Roberto Mancini amethibitisha kwamba straika Mario Balotelli amechoka kuvaa lenzi ya jicho na hivyo atafanyiwa upasuaji Jumanne  Septemba 4 kurekebisha jambo hilo.

Mancini amebainisha kwamba straika huyo Muitalia atafanyiwa upasuaji na hivyo hatacheza mechi ya leo dhidi ya QPR.

"Mario hayuko tayari kurejea uwanjani. Amechoka kuvaa lenzi. Anajisikia vyema sasa, lakini tatizo linaweza kumrejea wakati wowote," Mancini aliwaambia wanahabari.

Kocha huyo wa Man City tayari anamkosa straika wake mwingine Sergio Aguero ambaye atakuwa nje ya uwanja kwa wiki kadhaa baada ya kuumia katika mechi ya ufunguzi.

Alimtaka Balotelli kubeba jahazi katika kipindi ambacho Muargentina huyo yuko nje, lakini sasa Muitalia huyo naye amejumuika na Aguero nje ya uwanja.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 47 atalazimika sasa kutegemea ushirikiano wa Carlos Tevez na Edin Dzeko katika kuongoza mashambulizi.

No comments:

Post a Comment