Wednesday, August 15, 2012

ZITTO KABWE AHOJI: KWANINI SERIKALI INASEMA HAINA FEDHA KUWALIPA VIZURI WALIMU, MADAKTARI NA MANESI WAKATI KILA MWAKA HULIPA MISHAHARA HEWA ZAIDI YA SH. BILIONI 70?

Zitto Kabwe
Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Mhe. Zitto Kabwe ameitaka Serikali ieleze ni kwanini kila mwaka inalipa mishahara hewa inayofikia Sh. bilioni 70 na huku ikidai kwamba haina fedha za kutosha kuwalipa vizuri walimu, madaktari na manesi.

Mhe. Zitto ambaye pia ni waziri kivuli wa fedha, ameyasema hayo bungeni leo wakati akisoma hotuba ya kambi ya upinzani kuhusiana na wizara yake.


Alisema mishahara hiyo hewa inaonyesha kwamba serikali inazo fedha za kutosha kiasi cha kuwa na uwezo wa kuwalipa vizuri walimu, madaktari, manesi na watumishi wake wengine.

Akaitaka ichukue hatua ya kutokomeza mitandao ya kifisadi ili kuokoa mabilioni hayo ya fedha yanayopotea kila mwaka kupitia mishahara hewa. 

No comments:

Post a Comment