Wednesday, August 15, 2012

YAONE MAJEMBE MAPYA YA SIMBA

Beki wa kati wa timu ya taifa ya Kenya 'Harambee Stars', Patrick Ochieng akiwa ndani ya suti ya michezo ya Simba, Arusha leo. Ochieng na wachezaji wenzake wa Simba wanajiandaa na mechi ya kirafiki dhidi ya AFC Leopards ya Kenya.

Mshambuliaji raia wa Ghana, Daniel Akuffo akiwa katika 'track-suit' ya Simba mjini Arusha leo. Akuffo aliyejiunga na Simba kwa mkopo akitokea klabu ya Hearts of Oak na wachezaji wenzake wa Simba wanajiandaa na mechi ya kirafiki dhidi ya AFC Leopards ya Kenya.

Kocha msaidizi wa Simba, Amatre Richard (katikati) akipozi wachezaji wapya wa klabu hiyo, Patrick Ochieng (kushoto) na Daniel Akuffo mjini Arusha.

Nyota wapya wa Simba, Patrick Ochieng (kushoto) na Daniel Akuffo wakipozi kwa picha.

No comments:

Post a Comment