Wednesday, August 15, 2012

BOSI BARCELONA ATUA LONDON LEO KUZUNGUMZA NA ARSENAL JUU YA DAU LA KUMTWAA ALEX SONG

Alex Song
LONDON, England
Kiongozi wa juu kiutendaji wa klabu ya Barcelona, Josep Maria Bartomeu, ametua jijini London leo kukamilisha mazungumzo kuhusu dau wanalopaswa kulipa ili kumnasa kiungo wa Arsenal na timu ya taifa ya Cameroon, Alex Song.

Redio RAC-1 imesema leo kuwa Barca haiwezi tena kuendelea kusubiri hadi Arsenal iamue yenyewe kama iko tayari kumuuza Song ama la, na hivyo Bartomeu  ametua jijini London ili kuishinikiza iwauzie kiungo huyo.

Tayari Barca wameshaweka mezani dau la euro milioni 15 (Sh. bilioni 30) kwa ajili ya kiungo huyo wa kimataifa wa Cameroon, lakini Arsenal hawajawajibu chochote.

Arsenal wanadaiwa kuwa hawako tayari kumuachia Song kwa dau la chini ya euro milioni 20 (Sh. bilioni 40), wakati Barca wana matumaini ya kulalia bei ili wauziwe kiungo huyo mkabaji kwa euro milioni 18 (Sh. bilioni 35)

No comments:

Post a Comment