Friday, August 24, 2012

YANGA WAJIACHA NA RAIS KAGAME IKULU RWANDA

Kocha wa Yanga, Mbelgiji Tom Saintfiet (wa pili kushoto) akisalimiana na Rais Paul Kagame (kulia) wakati wachezaji na viongozi wa Yanga walipoitembelea Ikulu ya Rwanda
Rais wa Rwanda, Paul Kagame (kushoto) akimsikiliza Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Yusuph Manji (aliyesimama kulia) wakati wachezaji na viongozi wa Yanga walipoitembelea Ikulu ya Rwanda

Nahodha wa yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro' (kushoto) na kocha Tom Saintfiet (kulia) wakimwonyesha Rais wa Rwanda, Paul Kagame (katikati) kombe la ubingwa la Michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (maarufu Kombe la Kagame) wakati wachezaji na viongozi wa Yanga walipoitembelea Ikulu ya Rwanda.
Wachezaji na viongozi wa Yanga wakipozi na Rais wa Rwanda Paul Kagame wakati walipoitembelea Ikulu ya Rwanda.
Wachezaji wa Yanga wakipasha nchini Rwanda

Wachezaji wa Yanga wakipozi nje ya Jumba la Makumbusho la Kigali, Rwanda. PICHA ZOTE: SALEH ALLY WA CHAMPIONI

WACHEZAJI na viongozi wa klabu ya Yanga wameendelea na ziara yao nchini Rwanda ambapo sasa wamekutana na Rais Kagame katika Ikulu ya nchi hiyo mjini Kigali.

Yanga wamealikwa na Rais Kagame nchini Rwanda kwa ajili ya kupongezwa kufuatia kutwaa ubingwa wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (maarufu Kombe la Kagame), ambalo walilitetea kwa mara ya pili mfululizo. Lilikuwa ni kombe la tano kwa jumla kutwaliwa na Yanga, ambao sasa wanashika nafasi ya pili nyuma ya Simba wanaoshikilia rekodi ya wakati wote wakiwa wamelibeba mara sita.

Juzi mabingwa hao ambao walitetea ubingwa wao kwa kuifunga Azam ya jijini Dar es Salaam magoli 2-0 walikwenda kutembelea Jumba la Makumbusho ya Taifa ya Rwanda ambalo lina picha, silaha na vitu mbalimbali vinavyoonyesha maelfu wa nchi hiyo waliofariki kwenye mapigano ya yaliyotokea mwaka 1994.

Itakaporejea nchini wiki ijayo itaenda kuonana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete ambaye pia amewaalika kutokana na kuipeperusha vyema bendera ya nchi katika mashindano hayo yaliyofanyika nchini Julai.

Wakiwa Rwanda, Yanga wameungana kwa mara ya kwanza na beki wao mpya Mbuyu Twite aliyesajiliwa na klabu hiyo baada ya "kuuchana" mkataba aliousaini na mahasimu Simba.

No comments:

Post a Comment