Friday, August 24, 2012

CHELSEA YAKAMISHA USAJILI WA AZPILICUETA, VICTOR MOSES NAYE AELEKEA STAMFORD BRIDGE

Cesar Azpilicueta
Cesar Azpilicueta

Cesar Azpilicueta

CHELSEA wamemsajili beki Mhispania Cesar Azpilicueta kutoka Marseille, klabu hiyo ya Ligi Kuu ya England imesema leo.

"Beki mwenye umri wa miaka 22, ambaye hivi karibuni aliichezea timu ya taifa ya Hispania katika Michezo ya Olimpiki ya London, amewasili Stamford Bridge baada ya kuichezea Marseille kwa misimu miwili katika Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1)," Chelsea ilisema katika tovuti yao (www.chelseafc.com).

hakuna ada iliyotajwa ama muda wa mkataba aliosaini.

Azpilicueta alianza soka lake kwa kuichezea Osasuna, kabla ya kuondoka La Liga na kutua kwenye Ligue 1 mwaka 2010.

Wakati hajawahi kuichezea timu ya taifa ya wakubwa, amechezea timu za taifa za vijana za Hispania tangu alipoichezea timu yao ya U-16 mwaka 2005.

Azpilicueta ni mchezaji wa tano kusajili wa kocha Roberto Di Matteo katika kipindi hiki cha usajili baada ya Eden Hazard, Oscar, Marko Marin na Thorgan Hazard kutua Stamford Bridge.

Ni mchezaji wa nne Mhispania klabuni hapo pamoja na Juan Mata, Oriol Romeu na Fernando Torres.

Victor Moses (katikati) akipongezwa baada ya kuifungia goli Wigan wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England dhidi ya West Bromwich Albion kwenye Uwanja wa The Hawthorns Desemba 10, 2011 mjini West Bromwich, England.

Wigan Athletic ilitangaza jana kwamba imekubali ofa ya tano ya Chelsea ya kutaka kumsajili winga Victor Moses.

Mabingwa hao wa Ulaya wamekuwa wakimfuatilia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 raia wa Nigeria tangu mwisho wa msimu uliopita na hatimaye wamepewa ruhusa na Wigan kuzungumza na Moses.

"Klabu inathibitisha kwamba baada ya majaribio manne yaliyokwama kutoka Chelsea kwa ajili ya Victor Moses, ofa ya tano hatimaye leo imefikia viwango vilivyowekwa na Wigan Athletic na imekubaliwa," Wigan ilisema katika tovuti yao (www.wiganlactics.co.uk).

Chelsea imeshinda mechi zote mbili za kwanza za msimu.

No comments:

Post a Comment