Friday, August 24, 2012

BOLT ASHINDA TENA MITA 200, BLAKE ATISHA MITA 100, KIMWANA JELIMO WA KENYA BALAA DIAMOND LEAGUE

Mwanariadha wa Jamaica, Usain Bolt (kulia) akikimbia jirani na Mjamaica mwenzake Warren Weir wakati wa mbio za mita 200 za michuano ya Diamond League mjini Lausanne jana Agosti 23, 2012. Picha: REUTERS
Mwanariadha wa Jamaica, Usain Bolt akiviringika kushangilia ushindi wake wa mbio za mita 200 za michuano ya Diamond League mjini Lausanne jana Agosti 23, 2012. Picha: REUTERS

Mwanariadha wa Jamaica, Usain Bolt (kulia) akisalimia mashabiki baada ya kushinda mbio za mita 200 za michuano ya Diamond League mjini Lausanne jana Agosti 23, 2012. Picha: REUTERS
Mwanariadha wa Jamaica, Usain Bolt (katikati) akishangilia ushindi dhidi ya Mjamaica mwenzake Warren Weir na Wallace Spearmon wa Marekani wakati wa mbio za mita 200 za michuano ya Diamond League mjini Lausanne jana Agosti 23, 2012. Picha: REUTERS

Mwanariadha wa Jamaica, Usain Bolt (katikati) akishangilia ushindi dhidi ya Mjamaica mwenzake Warren Weir na Wallace Spearmon wa Marekani wakati wa mbio za mita 200 za michuano ya Diamond League mjini Lausanne jana Agosti 23, 2012. Picha: REUTERS
Mwanariadha wa Jamaica, Usain Bolt (katikati) akielekea kushinda dhidi ya Mjamaica mwenzake Warren Weir na Wallace Spearmon wa Marekani wakati wa mbio za mita 200 za michuano ya Diamond League mjini Lausanne jana Agosti 23, 2012. Picha: REUTERS
Mwanariadha wa Jamaica, Usain Bolt (wa pili kushoto) akichuana katika mbio za mita 200 za michuano ya Diamond League mjini Lausanne jana Agosti 23, 2012. Picha: REUTERS

Mwanariadha wa Jamaica, Yohan Blake akishangilia baada ya kushinda mbio za mita 100 za michuano ya Diamond League mjini Lausanne jana Agosti 23, 2012. Picha: REUTERS

Mwanariadha wa Jamaica, Yohan Blake akishangilia baada ya kushinda mbio za mita 100 za michuano ya Diamond League mjini Lausanne jana Agosti 23, 2012. Picha: REUTERS

Mwanariadha wa Jamaica, Yohan Blake (kulia) akishangilia baada ya kushinda dhidi ya Tyson Gay wa Marekani katika mbio za mita 100 za michuano ya Diamond League mjini Lausanne jana Agosti 23, 2012. Picha: REUTERS

Mwanariadha wa Kenya, Pamela Jelimo akishangilia ushindi wa mbio za mita 800 za michuano ya Diamond League mjini Lausanne jana Agosti 23, 2012. Picha: REUTERS

Mwanariadha wa Jamaica, Yohan Blake akielekea kushinda mbio za mita 100 za michuano ya Diamond League mjini Lausanne jana Agosti 23, 2012. Picha: REUTERS

LAUSANNE,
BINGWA wa Olimpiki, Usain Bolt alikimbia kwa muda wa sekunde 19.58 na kutwaa ubingwa wa mbio za mita 200 katika michuano ya Lausanne Diamond League Alhamisi wakati Yohan Blake aliifikia rekodi bora Na.3 ya kasi zaidi na kushinda mbio za mita 100 kwa kutumia sekunde 9.69.

Bolt kama kawaida yake alishangilia kwa staili yake marufu ya "gita la hewani" wakati akitambulishwa kwa mashabiki kabla ya kutawala mbio hizo kama ilivyotarajiwa, akishinda mbele ya Mholanzi Churandy Martina huku washindi watatu wote wakitumia chini ya sekunde 20.

Bolt, ambaye ambaye alisema lengo lake ni kumaliza msimu bila ya majeraha, alionekana kuridhishwa na matokeo yake ya karibuni.

"Inafurahisha, nilisikia muziki (kulele za mashabiki) na ilikuwa ni kwa ajili yangu, ilikuwa ni bab'kubwa," aliiambia televisheni ya BBC.

Mjamaica mwenzake Blake, ambaye alishinda medali ya fedha katika Olimpiki katika mita 100 na 200, alipiku rekodi yake binafsi kwa sekunde 0.06 wakati alipowasambaratisha magwiji wa mbio fupi duniani, Tyson Gay na Nesta Carter waliomfuatia.

Kiwango cha Blake kiliongeza hisia kwamba mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 22 ndiye mtu pekee anayeweza kuja kumpiku Bolt, ambaye ana umri wa miaka minne zaidi yake, ambaye alimshinda katika mbio zote za Michezo ya Olimpiki ya London.

Mariya Savinova, bingwa meingine wa Olimpiki, alibwagwa na Mkenya Pamela Jelimo katika mbio za wanawake za mita 800.

Savinova alikuwa sawa na Jelimo katika raundi ya mwisho na akawa akijiandaa kumpiku lakini Mkenya huyo ambaye alishika nafasi ya nne katika Olimpiki ya London, aliongeza kasi ghafla na Mrusi huyo hakuweza kumfikia.

No comments:

Post a Comment