Tuesday, August 7, 2012

VILANOVA HAMTAKI NEYMAR BARCELONA

Neymar
Tito Vilanova (kushoto) akishauriana na Pep Guardiola msimu uliopita kabla ya Guardiola hajaacha kazi ya kuifundisha Barca
Tito Vilanova (kushoto) akiwa na Pep Guardiola msimu uliopita kabla ya Guardiola hajaacha kazi ya kuifundisha Barca


KOCHA wa Barcelona, Tito Vilanova ameiambia bodi yake kwamba hamuhitaji nyota wa Santos, Neymar.

Gazeti la AS la Hispania limesema kuwa Vilanova anafurahia safu yake ya ushambuliaji kufuatia kurejea kwa David Villa aliyepona majeraha yake ya muda mrefu ya goti.

Kumekuwepo na uvumi wa Barca kutaka kumsajili Neymar baada ya Michezo ya Olimpiki, lakini Vilanova ameweka wazi kwamba hamuhitaji Mbrazil huyo kwa ajili ya msimu mpya.

No comments:

Post a Comment