Tuesday, August 7, 2012

BOLT: SITANII, NAOMBA KUSAJILIWA MAN UTD

Usain Bolt

MTU mwenye kasi zaidi duniani, Usain Bolt, anataka afanyiwe majaribio kwenye klabu ya Manchester United.

Bolt tayari ameshajihusisha na masuala ya soka baada ya kumpa mazoezi ya kukimbia Cristiano Ronaldo wakati wa maandalizi ya msimu mpya akiwa na United miaka kadhaa iliyopita.

"Watu wanadhani kwamba natania ninaposema kwamba nataka kuichezea Manchester United," alisema Mjamaica huyo.

"Lakini kama Alex Ferguson atanipigia simu na kusema, 'OK, njoo ufanye majaribio tuonekana uko vyema kiasi cha kutosha' itakuwa ngumu kwangu kusema hapana."

Bolt aliweka rekodi mpya ya mbio za mita 100 za Olimpiki Jumapili wakati alipotetea medali yake ya dhahabu akitumia muda wa sekunde 9.63, ambazo zilipiku rekodi yake aliyoiweka mwaka 2008 katika michezo ya Olimpiki ya Beijing, China.

No comments:

Post a Comment