Thursday, August 2, 2012

TUNDU LISSU AHOJI IDADI YA ABIRIA WALIOKUFA BAADA YA KUZAMA BOTI YA MV SKAGIT

Mhe. Tundu Lissu
Baadhi ya miili ya waliokufa katika ajali ya Mv Skagit ikishushwa baada ya kupatikana. 
Mv Skagit ilivyokuwa baada ya kupinduka huku baadhi ya abiria wakisubiri kuokolewa
Harakati za kuopoa miili ya watu waliokufa katika Mv Skagit zilivyokuwa.
Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Mhe. Tundu Lissu, amefufua upya sakata la kuzama kwa boti ya Mv Skagit kwa kutaka serikali ieleze ni watu wangapi hadi sasa waliothibitika kuwa wamekufa katika ajali hiyo iliyotokea Julai 18 katika eneo la Chumbe visiwani Zanzibar.

Akizungumza bungeni leo wakati akichangia mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Uchukuzi kwa mwaka ujao wa fedha, Mhe. Lissu alitaka kujua vilevile kama Mamlaka ya Udhibiti wa Usafirishaji wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) iliwahi kuikagua boti hiyo iliyozama Julai 18 wakati ikitokea jijini Dar es Salaam kuelekea Zanzibar.

"Kama jibu ndiyo, ni lini SUMATRA ilikagua? Na matokeo yake yalikuwaje?" Alihoji Mhe. Lissu, ambaye awali alisema kuwa SUMATRA inapaswa kuwa na taarifa za usalama wa boti zinazofanya safari zake kati ya Zanzibar na Bara.
 
Ilielezwa kuwa boti ya Skagit ilipigwa na dhoruba kali kabla ya kupinduka na kuzama yote chini kwa kina cha zaidi ya mita 60 huku ikiwa na watu zaidi ya 340.

No comments:

Post a Comment