Thursday, August 2, 2012

BARCELONA WAPANIA KUMNYAKUA ALEX SONG WA ARSENAL

*ETI WAJIPA MATUMAINI KUMNASA NDANI YA SAA 48

Alex Song akiwa katika 'uzi' mpya wa Arsenal wakati walipocheza dhidi ya Man City kwenye ziara yao ya China wiki iliyopita. Je, ni kweli atatimkia Barca kama alivyofanya Cesc Fabregas?

BARCELONA, Hispania
BARCELONA wanafanya kila wanaloweza ili kukamilisha mpango wa kumnasa kiungo Alex Song wa Arsenal kabla ya kumalizika kwa wikiendi, imefahamika.

Gazeti la michezo la Sport limesema kwamba Barca wangependa kumjumuisha ndani ya kikosi chao nyota huyo wa kimataifa wa Cameroon ndani ya saa 48 zijazo.

Inadaiwa kwamba pande zote mbili ziko tayari kukamilisha mpango huo, huku Arsenal wakiwa tayari kumuuza kwa paundi za England milioni 17, wakati Barca hadi sasa wameweka mezani ofa ya paundi za England milioni 12.

Inaelezwa kuwa Mkurugenzi wa Michezo wa Barca, Andoni Zubizarreta amehakikishiwa kwamba kocha wa Arsenal, Arsene Wenger hatakataa kumuuza Song ikiwa watafikia dau wanalolitaka.

No comments:

Post a Comment