Monday, August 27, 2012

TAZAMA UTAMBULISHO WA LUKA MODRIC ALIPOTUA REAL MADRID LEO... APEWA JEZI NA: 19, ASAINI MIAKA MITANO BAADA YA KUNUNULIWA KWA BILIONI 80/-... ASEMA ANA USONGO KUIVAA BARCELONA JUMATANO!

Niko fiti jamani...! Hapa 'jembe' Modric likichukuliwa vipimo vya afya jijini Madrid leo asubuhi.
Yaaaap...si mnaona wenyewe, mi niko ngangari kinoma! 


Mimi jembe la ukweli Luka Modric... nimekubali kusaini mkataba wa miaka mitano kuichezea Real Madrid kwa malipo ya mshahara mnono lakini lazima tuifunge Barcelona kila mimi niwapo uwanjani...! Kiungo Luka Modric (kushoto) akisaini mkataba wa kuichezea Real Madrid leo, akiwa na rais wa klabu yake mpya, Florentino Perez a.k.a "pedezyee nyamihela", "mutu ya fweza"', "mopao"     
Waleteni hao Barcelona... Luka Modric akionyesha 'maujuzi' baada ya kutambulishwa rasmi katika klabu yake mpya ya Real Madrid kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu leo.

Daddy na mi nawedha...! Luka Modric akionyesha "mautundu" na mtoto wake wa kiume wakati wa utambulisho katika klabu yake mpya ya Real Madrid kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu leo.  
Luka Modric

Hapa mtasuuzika tu... Luka Modric akiwa kwenye Uwanja wa Bernabeu.

Nirudi tena Tottenham? Ha ha haaa...! Luka Modric akiendelea kutambulishwa kwenye uwanja wa Real Madrid, Santiago Bernabeu.

Ms'konde wana Madridistas... Luka Modric ndani ya Uwanja wa Santiago Bernabeu wakati akitambulishwa baada ya kukamilisha usajili wake Real Madrid.
MADRID, Hispania
Real Madrid wamekamilisha usajili wa kiungo mchezeshaji wa timu ya taifa ya Croatia, Luka Modric kutoka Tottenham Hotspur leo na kujipa matumaini ya kufanya vizuri baada ya kuanza vibaya msimu wa La Liga, Ligi Kuu ya Hispania.

Modric alitua Madrid leo asubuhi na kufuzu vipimo vya afya kabla ya kusaini mkataba wa kuichezea kwa miaka mitano mbele ya rais anayesifika kwa kumwaga fedha wa Real Madrid, Florentino Perez, na kisha akazungumza katika mkutano na waandishi wa habari kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu.

Kiungo huyo mwenye miaka 26, ambaye alikabidhiwa jezi Na. 19, alisema kuwa amefurahi kutua Real Madrid na kwamba atajitahidi kuonyesha kiwango cha juu ili apate nafasi ya kupangwa katika kikosi cha kwanza cha kocha Jose Mourinho.

"Nitalazimika kujituma sana ili kupata namba katika kikosi cha kwanza cha wachezaji 11... nimejiandaa kwa hilo," aliwaambia waandishi huku akitazamwa na mkewe na mtoto wake wa kiume.

"Nimekuja hapa kuimarika kila uchao na kutwaa mataji nikiwa na Real Madrid. Haya ndio malengo yangu," aliongeza.

"Naamini kwamba nina vitu vinavyonifanya nistahili kuichezea timu hii. Nina kila kitu ninachohitaji na hivyo nataka nifaidi kucheza soka na pia kujifunza zaidi.

"Nawashukuru Tottenham, lakini sasa nafungua ukurasa mpya katika maisha yangu."

Wakati hakuna klabu yoyote kati ya hizo iliyotoa taarifa ya kifedha kuhusiana na uhamisho huo, vyombo vya habari vya Hispania vimeripoti kuwa Real wanalipa euro milioni 35 (Sh. bilioni 68) taslim na ziada ya euro milioni 7 zikitarajiwa kulipwa ikiwa Modric ataipa mafanikio klabu hiyo, hivyo gharama za jumla kufikia euro milioni 42 (Sh. bilioni 80).

Real watacheza dhidi ya Barcelona keshikutwa Jumatano katika mechi ya marudiano  kuwania taji la Super Cup kwenye Uwanja wa Bernabeu na Modric amesema kuwa anatamani kuwemo kikosini ili naye afaidi utamu wa 'el clasico'.

"Real dhidi ya Barca ni miongoni mwa mechi kali na zenye msisimko zaidi duniani na hivyo ningependa kucheza, lakini ni kocha ndiye atakayeamua," amesema Modric.

No comments:

Post a Comment