Sunday, August 19, 2012

STRAIKA YAWATAKIA IDD MUBARAK WADAU WOTE

Wanawake wa Thailand wakiswali swala ya Idd katika msikiti wa Grue Sae katika kitongoji cha Pattani, kusini mwa Thailand leo asubuhi Agosti 19, 2012. Picha: REUTERS
Waafghanistan wakishiriki swala ya Idd nje ya msikiti wa Shah-e Doh Shamshira mjini Kabul leo asubuhi Agosti 19, 2012. Picha: REUTERS
Waislamu wakiomba dua baada ya swala ya Eid al-Fitr mjini Moscow leo Agosti 19, 2012. Picha: REUTERS
Waislamu wakihudhuria swala ya Idd mjini Moscow leo Agosti 19, 2012. Picha: REUTERS
Waafghanistan wakishiriki swala ya Idd nje ya msikiti wa Shah-e Doh Shamshira mjini Kabul leo asubuhi Agosti 19, 2012. Picha: REUTERS
Njiwa wakiruka wakati wakazi wakiswali swala ya Idd nnje ya msikiti wa Shah-e Doh Shamshira mjini Kabul leo asubuhi Agosti 19, 2012. Picha: REUTERS
Wanaume wakishiriki swala ya Idd katika Msikiti wa Grand mjini Riyadh leo asubuhi. Picha: REUTERS
Watoto wakiswali swala ya Idd na baba zao nje ya msikiti mjini Cairo, Misri leo Agosti 19, 2012. Picha: REUTERS
Wanaume wakishiriki swala ya Idd mjini Riyadh leo asubuhi. Picha: REUTERS
Mtoto akiangalia kamera wakati wakimbizi wa Syria na wakazi wakiswali swala ya Idd nje ya ubalozi wao mjini Amman leo asubuhi Agosti 19, 2012. Picha: REUTERS
Binti Muislamu wa Thailand akisimama nje ya msikiti wa Grue Sae uliopo katika kitongoji cha Pattani, kusini mwa Thailand leo Agosti 19, 2012. Picha: REUTERS

BLOGU ya STRAIKA inaungana na Waislamu kote duniani kuwatakia Sikukuu njema ya IDD EL FITR.

Tule, tunywe (sio pombe kwa sababu Uislamu unakataza pombe), tuvae, tufurahi, tutembelee ndugu na jamaa, wagonjwa hospitalini na tuwasaidie wenye kuhitaji na Mungu atatulipa.

No comments:

Post a Comment