Sunday, August 19, 2012

SONG KUPIMA AFYA BARCA KESHO, KUSAINI MIAKA MITANO

Alex Song
Alex Song akizungumza na wanahabari wakati wa ziara ya Arsenal ya kujiandaa na msimu huu barani Asia ambapo walicheza dhidi ya Kitchee FC kwenye Uwanja wa Hong Kong Julai 29, 2012.


BARCELONA wametangaza kuafikiana bei ya paundi milioni 15 kwa ajili ya kumsajili kiungo wa Arsenal, Alex Song.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24 raia wa Cameroon sasa atasafiri kwenda Nou Camp kuafikiana malipo binafsi na kupimwa afya, Arsenal ilitangaza katika taarifa yake iliyowekwa kwenye tovuti yao.

Taarifa ya Barcelona ilisema: "Barcelona wameafikiana dili na Arsenal kwa ajili ya uhamisho wa kiungo Alex Song kwenda Nou Camp. Ada ya Euro milioni 19 (paundi milioni 15).

"Kiungo wa kimataifa wa Cameroon atasaini mkataba wa miaka mitano wenye kipengele cha kuvunjia mkataba cha euro milioni 80.

"Jumatatu (kesho) atafanyiwa vipimo vya afya na kisha atajiunga na wachezaji wenzake kwa ajili ya kutambulishwa rasmi."

No comments:

Post a Comment