Sunday, August 19, 2012

KILA KOMBE JIPYA NI LA SIMBA

Wachezaji wa timu B ya Simba wakishangilia ubingwa wa Ligi ya Super8 baada ya kuifunga timu ya wakubwa ya Mtibwa Sugar kwa magoli 4-3, huku nyoa anayeinukia vyema, Christopher Edward akifunga hat-trick na kuwa mfungaji bora baada ya kufikisha magoli 8 katika mechi 5 za michuano hiyo mipya iliyofanyika kwa mara ya kwanza ya kujiandaa na msimu mpya kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana. Pamoja na kombe la ubingwa, Simba pia imeondoka na zawadi ya Sh. milioni 40 huku Mtibwa wakipata zawadi ya pili ya Sh. milioni 20 kutoka kwa wadhamini wa michuano BancABC. TFF, Shirikisho la soka nchini limesaini mkataba wa miaka mitatu wa kuendesha ligi hiyo inayohusisha timu nane, nne kutoka Bara nne Zanzibar. Kabla ya kushiriki kombe la Kagame, Simba ilitwaa kombe jipyaya Urafiki lililofanyika mjini Zanzibar. Timu ya vijana ya Simba imeonyesha uwezo mkubwa baada ya pia "kuwakalisha" watu wazima wa Azam, ambao walichezasha wachezaji wa timu A ya Ligi Kuu ya Tanzania bara katika mechi yao ya nusu fainali. Simba oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!

No comments:

Post a Comment