Sunday, August 19, 2012

PARDEW ASUKUMA MWAMUZI

Kocha wa Newcastle, Alan Pardew (kulia) akimbwatukia mshika kibendera Stuart Burt wakati wa mechi yao dhidi ya Tottenham jana Jumamosi.

KOCHA wa Newcastle, Alan Pardew ameomba radhi kwa kumsukuma mshika kibendera wakati wa mechi yao waliyoshinda 2-1 dhidi ya Tottenham juzi. 

Penalti ya dakika za lala salama ya Hatem Ben Arfa iliwapa Newcastle pointi 3 baada ya Jermain Defoe kusawazisha goli kali lililofungwa na Demba Ba. 

Lakini Pardew alipewa kadi nyekundu baada ya kumsukuma mshika kibendera Stuart Burt wakati akilalamikia mpira uliotoka wakati wa shambulizi la Spurs. 

"Tumefurahi kwa ushindi, lakini ni aibu kwangu kwa nilichofanya," alisema.

No comments:

Post a Comment