Wednesday, August 1, 2012

SNOOP DOGG AACHA RAP NA KUGEUKIA REGGAE, SASA ABADILI JINA NA KUJIITA “SNOOP LION”


Sasa naitwa Snoop Lion...msanii Snoop Dogg akijiweka kwa pozi la picha jijini New York juzi  baada ya kutangaza kubadili jina lake.
Baada ya kumkamata mpakani akiwa na misokoto ya bangi, maafisa uhamiaji wa Norway waliwahi kumpiga marufuku kwa miaka miwili kuingia tena nchini mwao msanii aliyekuwa akifahamika awali kwa jina la Snoop Dogg.

Hata hivyo, maafisa hao wa Norway hawawezi kumzuia rapa huyo kubadili jina lake na sasa kujiita Snoop Lion.

Msanii huyo alitangaza juzi kuwa anabadili jina lake la awali ikiwa ni sehemu ya mikakati aliyo nayo sasa ya kujitambulisha kwa mashabiki kama nyota wa muziki wa reggae.

"Si nia yangu kuwavunjia heshima marapa wengine, lakini kamwe hawawezi kushindana na mimi katika rap," alisema wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini New York juzi.

"Nimeshinda kila tuzo ambayo msanii nyota anaweza kuipata katika muziki wa rap, katika rap wananiita 'Mjomba Snoop' . Wakati unapofikia hadhi ya kuitwa mjomba, ni vizuri sasa kugeukia kitu kingine."

Kutokana na jina lake la sasa, baadhi ya watu, akiwamo Dk. Ruth,  wamekuwa wakitania kwamba kuna siku msanii huyo ataiga jina la mijusi mikubwa na ya kutisha ya kale aina ya dinosaur na kujiita “Snoop Tyrannosaurus Rex”.

No comments:

Post a Comment