Friday, August 31, 2012

SINCLAIR ALIYEKUWA MPISHI WA PASI KALI ZA SWANSEA ASAJILIWA RASMI MAN CITY LEO... ACHEKELEA KLABU YAKE MPYA KUPANGWA NA REAL MADRID YA AKINA CRISTIANO RONALDO KATIKA KLABU BINGWA ULAYA, KESHO KUCHEZA DHIDI YA QPR LIGI KUU YA ENGLAND

Yaaap.... waleteni hao Real Madrid! Sinclair akionyesha jezi yake baada ya kutua Man City leo.
MANCHESTER CITY, England
Winga nyota wa Swansea na timu ya Himaya ya England iliyoshiriki michezo ya Olimpiki jijini London 2012, Sinclair (23), amejiunga rasmi na klabu ya Manchester City leo na anaweza kupangwa katika mechi yao ya kesho ya Ligi Kuu ya England dhidi ya QPR.

Straika huyo alionyesha kiwango cha juu akiwa na Swansea msimu uliopita, na pia aliisaidia timu yake hiyo ya zamani kupanda katika Ligi Kuu ya England msimu mmoja kabla.

"Nimefurahi kuona kila kitu kikienda kama kilivyopangwa na sasa mimi ni mchezaji wa Man City," amesema Sinclair.

"Kuna wakati nilifikiri kwamba jambo kama hili haliwezi kutokea, kwahiyo sasa nimefurahi sana na, nina usongo wa kuanza kuitumikia.

"Ni raha sana kucheza pamoja na wachezaji nyota duniani na wakati ninapoona kuwa tutacheza mechi mbili katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid najikuta nikihisi kama tuko katika sayari nyingine, ni furaha tupu."

Sinclair alianza soka katika klabu ya Bristol Rovers na kucheza mechi yake ya kwanza akiwa na miaka 15 kabla kuhamia Chelsea alikodumu kwa miaka mitano.

Aliuzwa mfululizo kwa mkopo katika kipindi chake cha kuwa Chelsea, akizichezea Plymouth, QPR, Charlton, Crystal Palace, Birmingham na Wigan kabla ya kutwaliwa jumla na Swansea msimu wa 2010 kwa dau poa la paundi za England 500,000.

Sinclair alikuwa mhimili wa kikosi cha Himaya ya England katika michuano ya Olimpiki London 2012, akicheza mechi nne na kufunga goli moja.

No comments:

Post a Comment