Friday, August 31, 2012

MAICON ATUA MAN CITY LEO AKITOKEA INTER MILAN


MANCHESTER CITY, England
Klabu ya Manchester City inayoshikilia ubingwa wa Ligi Kuu ya England imethibitisha leo kumnasa beki wa kulia, Douglas Maicon kutoka katika klabu ya Inter Milan inayoshiriki Serie A, Ligi Kuu ya Italia.

Beki huyo mwenye miaka 31 anatarajiwa kuleta uzoefu wake wa mechi za kimataifa na Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwenye kikosi cha Man City, kwani tayari ameshashiriki fainali za Kombe la Dunia na pia kubeba taji la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya msimu wa 2009.

"Beki Maicon wa Brazili amejiunga Manchester City kwa mkataba wa kudumu," imesema taarifa ya Man City iliyotolewa leo kupitia tovuti yao rasmi.

"Beki huyu wa kulia anahamia Man City akitokea Inter Milan kwa ada isiyotajwa."

No comments:

Post a Comment