Sunday, August 19, 2012

SHEIKH NURDIN KISHKI ALAANI TABIA YA KUSHEREHEKEA IDDI KWA DISKO, NGOMA, MUZIKI WA DANSI, ULEVI, ZINAA... !

Sheikh Nurdin Kishki akitoa mawaidha kwa waumini wa Kiislamu baada ya kumalizika kwa swala ya Idi kwenye viwanja vya Tandika Mwembe -Yanga jijini Dar es Salaam, leo.

Baadhi ya waumini wa Kiislamu wakisikiliza mawaidha kutoka kwa Sheikh Nurdin Kishki kwenye viwanja vya Tandika Mwembe -Yanga jijini Dar es Salaam, leo.

Sehemu ya mamia ya waumini wa Kiislamu wakifuatilia mawaida kutoka kwa Sheikh Nurdin Kishki kwenye viwanja vya Tandika Mwembe -Yanga jijini Dar es Salaam, leo.

Baadhi ya akina mama wakisikiliza mawaidha na wengine wakiondoka baada ya kuswali Idi kwenye viwanja vya Tandika Mwembe -Yanga jijini Dar es Salaam, leo.

Baadhi ya akina mama wakisikiliza mawaida kutoka kwa Sheikh Nurdin Kishki baada ya kumalizika kwa swala ya Idi kwenye viwanja vya Tandika Mwembe -Yanga jijini Dar es Salaam, leo.

Haa haa haaaa....leo ni ubwabwa tu! Mtoto Muzzammil akionekana mwenye furaha tele baada ya kumalizika kwa swala ya Idi kwenye viwanja vya Tandika Mwembe -Yanga jijini Dar es Salaam, leo.

Halo halooo....! Watoto hawa pia walikuwa wenye furaha baada ya kumalizika kwa swala ya Idi kwenye kwenye viwanja vya Tandika Mwembe -Yanga jijini Dar es Salaam, leo.

Watoto Luqman (kulia) na mdogo wake Muzzammil wakijiandaa kurejea kwao baada ya kumalizika kwa swala ya Idi kwenye viwanja vya Tandika Mwembe -Yanga jijini Dar es Salaam, leo.

Leo pilau tu...! Mtoto huyu anaonekana kama anayetafakari baada ya kumalizika kwa swala ya Idi kwenye viwanja vya Tandika Mwembe -Yanga jijini Dar es Salaam, leo.

Waumini wa dini ya Kiislamu wakiswali swala ya Idi kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.

Waumini akina mama wakiwa kwenye swala ya Idi visiwani Zanzibar leo.

Makamu wa Rais, Dk. Ghalib Mohamed Bilal akizungumza na waumini baada ya swala ya Idi kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.

Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi (kulia) akisalimiana na waumini baada ya kumalizika kwa swala ya Idi kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar,Maalim Seif Shariff Hamad (wa nne kushoto) akiswali Idi visiwani Zanzibar leo. Wa pili kushoto ni Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mhe. Pandu Ameir Kificho.   

Mufti wa Tanzania, Sheikh Shaaban Issa Simba akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu wakati wa swala ya Idi iliyofanyika kitaifa mkoani Ruvuma leo.

Bango linaloashiria onyesho katika siku ya Idi leo katika ukumbi mmoja uliopo Tandika Maguruwe jijini Dar es Salaam leo... kusherehekea Idi kwa mtindo huu ndiko kulikokatazwa na Sheikh Kishki leo. 

Tangazo hili nalo nd'o yaleyale yanayolaaniwa na Sheikh Kishki kwani mwishowe huambatana na matendo ya kumkufuru Mwenyezi Mungu... hapa ni katika ukumbi mmoja uliopo Tandika Maguruwe jijini Dar es Salaam.
Mhadhiri maarufu wa dini ya Kiislamu nchini, Sheikh Nurdin Kishki, amelaani tabia ya kusherehekea sikukuu ya Idi kwa matamasha hafla na matamasha 'kharamu' ya ngoma, disco, muziki wa dansi, taarabu, bongofleva, ulevi, zinaa na matendo mengine yanayokwenda kinyume na mafundisho ya dini hiyo.

Akizungumza na mamia ya waumini walioshiriki ibada ya swal ya Idi kwenye viwanja vya Tandika Mwembe-Yanga leo asubuhi, Sheikh Kishki alisema kuwa kusherehekea sikukuu ya Idi kwa vitendo vya aina hiyo ni makosa makubwa na kwamba humchukiza Allah, Muumba wa Mbingu na Ardhi.

"Wamelaaniwa wale wote wanaosherehekea sikukuu hii kwa matendo maovu," alisema Sheikh Kishki.

"Hawa wanaofanya vitendo vya kumuudhi Mwneyezi Mungu katika siku kama ya leo wajiandae kwa adhabu kali siku ya kiama... tuwaombee dua ili waache na wale watakaoendelea basi wajiandae kupata laana za Mwenyezi Mungu," alisema Sheikh Kishki.

Katika hatua nyingine, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Ghalib Mohamed Bilal, amewaombaa waumini wa dini ya Kiislamu kushiriki katika zoezi la sensa kwani ni muhimu kwa maendeleo ya taifa.

Dk. Bilal aliyasema hayo baada ya swala ya Idi kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Hivi karibuni, wanaharakati kadhaa wa Kiislamu, akiwemo Sheikh Ponda Issa Ponda, wamekaririwa mara kadhaa wakisema kuwa Waislamu hawatashiriki sensa ikiwa katika madodoso hakutakuwa na kipengele cha dini. Ponda na wanaharakati wenzake waliamua kutangaza msimamo huo baada ya hivi karibuni, Televisheni ya Taifa (TBC1) kuutangazia umma wakati wa sherehe za miaka 50 ya uhuru kuwa nchi hii ina Wakristo asilimia 52, Waislamu asilimia 32 na watu wa dini nyingine asilimia 14; takwimu ambazo zilibainika kuwa ni za kupikwa kwani hakuna sensa yoyote iliyowahi kufanywa nchini na kuonyesha matokeo ya aina hiyo.

Ili kukomesha vitendo vya aina hiyo, ndipo Sheikh Ponda na wanaharakati wengine ambao wanaamini Waislamu ndio wengi zaidi walipoitaka Serikali iweke kipengele cha dini katika madodoso ya sensa ili kujua ukweli ni watu wa dini gani walio na idadi kubwa zaidi nchini.

Hata hivyo, TBC kupitia mkurugenzi wake Clement Mshana ilishaomba radhi kutokana na upotoshwaji uliofanywa na kituo hicho, ikisema kwamba mhusika aliyetoa taarifa hizo potofu ameshachukuliwa hatua ya kuonywa.

Swala ya Idi kitaifa leo iliswaliwa mkoani Ruvuma ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Mufti Shaaban Issa Simba. 

No comments:

Post a Comment