Thursday, August 2, 2012

SEYDOU KEITA AMSHUKIA PEP GUARDIOLA

Kocha Pep Guardiola (kulia) akifuatiliamechi wakati akimuingiza uwanjani Seydou Keita (kushoto) wakati wa mechi yao ya La Liga dhidi ya Athletic Bilbao kwenye Uwaja wa Camp Nou Machi 31, 2012 mjini Barcelona, Hispania.

KIUNGO wa klabu ya Dalian Aerbin ya nchini China, Seydou Keita amesema anaona kocha wa zamani wa Barcelona, Pep Guardiola hakuwa muwazi kwake. Keita amesisitiza kwamba hakuondoka Barca ili kufuata pesa China. Aliliambia gazeti la Match la nchini Mali: "Nimesikia mara nyingi sana kwamba nilikuwa napendwa na Guardiola. 


"Aliponizungumzia vyema kwa watu wa habari, nilidhani kila kitu kiko poa. Lakini kisha hakunichezesha. 


"Ninachojutia ni kwamba alikuwa akinisifu kwa watu, lakini hanijumuishi kwenye kikosi (kwa kwanza). Alipaswa kuzungumza nami uso kwa uso."

No comments:

Post a Comment