Friday, August 10, 2012

SAA YA BEI KALI YA BLAKE YA SH. MIL 775 YAIKERA KAMATI YA OLIMPIKI

Yohan Blake (kushoto) akikimbia mbio za mchujo huku akionyesha saa yake ya bei mbaya mkononi.
Yohan Blake (katikati) akikimbia mbio za mchujo huku akionyesha saa yake ya bei mbaya mkononi.
Yohan Blake akikimbia mbio za mchujo huku akionyesha saa yake ya bei mbaya mkononi.
Vampire? Blake anavyopenda kufanya wakati akitambulishwa kabla ya kuanza mbio
Braza wewe unanishinda kwa hatua tu, ningekuwa mrefu kama wewe usingeniweza... Blake (kushoto) akimpongeza Mjamaica mwenzake Bolt baada ya kushinda mita 200 katika Michezo ya Olimpiki 

Fainali.. wanaume wakiondoka kwenye line

MAOFISA wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) wamekerwa na saa ya bei kali iliyovaliwa na mwanariadha wa Jamaica, Yohan Blake, wakati akishiriki mbio za mita 100 na 200 za Olimpiki ya London 2012.

Blake alivaa saa hiyo yenye thamani ya dola za Marekani 500,000 (sawa na Sh. milioni 775), na IOC haijafurahishwa na jambo hilo.

Kwa mujibu wa ripoti ya jarida la TNT la Uingereza pamoja na vyanzo vingine kadhaa vya Uingereza, saa hiyo, ambayo inaonekana katika picha kwenye mkono wa kulia wa Blake, ni saa maalum ya kimichezo iliyonakishiwa na rangi za kijani na njano za rangi ya bendera ya Jamaica.

Saa hiyo ambayo inaitwa Richard Mille Tourbillion, ilibuniwa maalum kwa ajili ya Blake kuivaa katika Michezo ya Olimpiki.

Wakati maafisa wanaona kwamba Blake alikuwa akifanya matangazo ya biashara, nyota huyo aliendelea kuivaa katika mbio za mita 200, ambazo nazo alimaliza akishika Na.2 nyuma ya Mjamaica mwenzake Usain Bolt, kama ilivyokuwa katika mbio za mita 100.

No comments:

Post a Comment