Tuesday, August 21, 2012

RVP AHAMISHIA MIKOSI YAKE YA ARSENAL MAN UTD, WAANZA NA KICHAPO

Nimeleta mikosi ya Arsenal huku... Straika mpya wa Manchester United, Robin van Persie akijiuliza kwenye benchi la timu hiyo kabla ya kuingia uwanjani wakati timu yake ikiwa nyuma 1-0 dhidi ya Everton katika mechi yao ya ufunguzi wa Ligi Kuu ya England kwenye Goodison Park mjini Liverpool jana Agosti 20, 2012. Man U 'walikalishwa' 1-0. Picha: REUTERS
Straika mpya wa Manchester United, Robin van Persie akiwa hoi wakati wa mechi yao ya ufunguzi wa Ligi Kuu ya England dhidi ya Everton kwenye Uwanja wa Goodison Park mjini Liverpool, kaskazini mwa England jana Agosti 20, 2012. Man United "walikalishwa" 1-0 kwa bao la Marouane Fellaini. Picha: REUTERS
Muuaji wa Mashetani.... Marouane Fellaini wa Everton (katikati) akishangilia goli lake dhidi ya Manchester United wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Goodison Park mjini Liverpool, kaskazini mwa England jana Agosti 20, 2012. Picha: REUTERS
Tumeua mashetani kisha tunatambulisha mashine mpya.... mchezaji mpya wa Everton, Kevin Mirallas akipozi kwa picha wakati wa utambulisho jana kwenye Uwanja wa Goodison Park mjini Liverpool, ambapo Man United walikalishwa 1-0. Picha: REUTERS

No comments:

Post a Comment