Thursday, August 2, 2012

REAL MADRID YAWAPIKU MATAJIRI ANZHI KATIKA MBIO ZA KUMSAJILI WINGA LUIS NANI WA MAN U

Luis Nani
MADRID, Hispania
REAL Madrid wamejitosa katika mbio za kumuwania winga Luis Nani wa Manchester United na taarifa zinadai kwamba hivi sasa wanapewa nafasi kubwa ya kumpata dhidi ya wapinzani wao katika vita hiyo, klabu ya Anzhi ya Urusi.

Imeelezwa kwamba Real wana matumaini ya kumnasa winga huyo wa kimataifa wa Ureno kwavile hadi sasa amegoma kusaini mkataba mpya ili aendelee kubaki katika klabu yake ya sasa ya Man U.

Taarifa zimeeleza zaidi kwamba, kutofikia makubaliano kwa Nani na Man U ndiko kunakojenga imani kuwa klabu yake haitakataa kumuuza katika kipindi hiki cha uhamisho wa majira ya kiangazi.

Kocha wa Real, Jose Mourinho anasimamiwa na wakala huyo huyo wa Nani, ambaye ni Jorge Mendes, na inaelezwa zaidi kwamba ameongeza kasi ya kumtaka winga huyo.

No comments:

Post a Comment