Thursday, August 2, 2012

MAN CITY SASA WAMFUNGIA KAZI DAVID LUIZ WA CHELSEA

David Luiz
LONDON, England
MANCHESTER City ni miongoni mwa klabu zilizojitokeza kumfukuzia beki David Luiz wa Chelsea, imefahamika.

Imeelezwa na mtandao wa Mercato365 kwamba, kocha wa Man City, Roberto Mancini, amedhamiria kusajili beki mpya wa kati na anayemtaka kwa ni David Luiz.

Tayari Mancini ameshakataliwa ofa yake ya paundi za England milioni 13 na milioni 16 alizotuma awali kwa Liverpool ili kumpata beki Dan Agger.

Luiz anaweza kujikuta akitamani kuondoka Chelsea baada ya kuona kwamba hana nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha timu yake katika msimu ujao wa Ligi Kuu ya England kwani kocha Roberto di Matteo atawategemea zaidi mabeki wa kati 'pacha', John Terry na Gary Cahill.

Inatarajiwa kuwa Man City watazidi kuongeza shinikizo la kumsajili Luiz, hata kama mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich hayuko tayari kufanya biashara hiyo.

No comments:

Post a Comment