Thursday, August 30, 2012

REAL MADRID YATWAA SUPERCUP HISPANIA... RONALDO, MESSI WAFUNGA MABAO YA VIDEO, BARCELONA HOI WAMALIZA 10 BAADA YA ADRIANO KULA NYEKUNDU KIPINDI CHA KWANZA,

Tumetishaaaaaa...... Kipa wa Real Madrid, Iker Casillas (kulia) na wachezaji wenzake wa wakishangilia na kombe baada ya kushinda mechi yao ya marudiano ya Super Cup dhidi ya Barcelona kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid Agosti 30, 2012. Picha: REUTERS
Wachezaji wa Real Madrid, Pepe (kushoto) na Cristiano Ronaldo wakishangilia na kombe baada ya kushinda mechi yao ya marudiano ya Super Cup dhidi ya Barcelona kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid Agosti 30, 2012. Picha: REUTERS
Straika wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo akishangilia baada ya kushinda mechi yao ya marudiano ya Super Cup dhidi ya Barcelona kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid Agosti 30, 2012. Picha: REUTERS
Wachezaji wa Real Madrid wakishangilia na kombe baada ya kushinda mechi yao ya marudiano ya Super Cup dhidi ya Barcelona kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid Agosti 30, 2012. Picha: REUTERS
Kipa wa Real Madrid, Iker Casillas akiinua kombe baada ya kushinda mechi yao ya marudiano ya Super Cup dhidi ya Barcelona kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid Agosti 30, 2012. Picha: REUTERS

Straika wa Barcelona, Lionel Messi akipiga 'fri-kiki' na kufunga  wakati wa mechi yao ya marudiano ya Super Cup kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid Agosti 30, 2012. Picha: REUTERS

Kipa wa Real Madrid, Iker Casillas akishindwa kuokoa 'fri-kiki' ya hatari iliyopigwa na straika wa Barcelona, Lionel Messi wakati wa mechi yao ya marudiano ya Super Cup kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid Agosti 30, 2012. Picha: REUTERS
Straika wa Real Madrid, Gonzalo Higuain (katikati) akifunga goli dhidi ya kipa wa Barcelona, Victor Valdes wakati wa mechi yao ya marudiano ya Super Cup kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid Agosti 30, 2012. Picha: REUTERS
Straika wa Barcelona, Lionel Messi (katikati) akishangilia goli lake dhidi ya Real Madrid pamoja na mchezaji mwenzake Xavi Hernandez wakati wa mechi yao ya marudiano ya Super Cup kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid Agosti 30, 2012. Picha: REUTERS
Hongera kaka, mmetisha...... kipa wa Barcelona, Victor Valdes (aliyeipa mgongo kamera) akimpongeza straika wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo baada ya kushinda mechi yao ya marudiano ya Super Cup kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid Agosti 30, 2012. Picha: REUTERS
Hoiiiii.... chezea Mourinho wewe? ...... Straika wa Barcelona, Lionel Messi akijiuliza baada ya Real Madrid kufunga goli la pili wakati wa mechi yao ya marudiano ya Super Cup kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid Agosti 30, 2012. Picha: REUTERS
Dakika 15 tu nimebeba kombe kweli kuchezea hii timu raha.... Kiungo mpya wa Real Madrid, Luka Modric akishangilia baada ya kushinda mechi yao ya marudiano ya Super Cup dhidi ya Barcelona kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid Agosti 30, 2012. Picha: REUTERS

Kaka umetubania sana hongera, ila ile 'fri-kiki' kauguze mbavu.... Straika wa Barcelona, Lionel Messi (kushoto) akimpongeza kipa wa Real Madrid, Iker Casillas baada ya mechi yao ya marudiano ya Super Cup kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid Agosti 30, 2012. Picha: REUTERS
Kaka umetubania sana hongera, ila ile 'fri-kiki' kauguze mbavu.... Straika wa Barcelona, Lionel Messi (kushoto) akimpongeza kipa wa Real Madrid, Iker Casillas baada ya mechi yao ya marudiano ya Super Cup kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid Agosti 30, 2012. Picha: REUTERS

Straika wa Real Madrid, Gonzalo Higuain (katikati) akifunga goli dhidi ya kipa wa Barcelona, Victor Valdes wakati wa mechi yao ya marudiano ya Super Cup kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid Agosti 30, 2012. Picha: REUTERS

Straika wa Real Madrid, Gonzalo Higuain akishangilia goli lake alilofunga dhidi ya Barcelona wakati wa mechi yao ya marudiano ya Super Cup kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid Agosti 30, 2012. Picha: REUTERS
Bonge la rekodi. Mechi tano za El Classico magoli matano.... Straika wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo (kushoto) akishangilia goli lake dhidi ya Barcelona pamoja na mchezaji mwenzake Di Maria wakati wa mechi yao ya marudiano ya Super Cup kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid Agosti 30, 2012. Ronaldo amefikia rekodi ya wakati wote ya kufunga magoli matano katika mechi tano mfululizo za Classico. Na katika mechi saba zilizopita za Classico, Ronaldo kafunga magoli 6. Chezea CR7 wewe?.... Picha: REUTERS
MADRID, Hispania
KOCHA wa Barcelona, Tito Vilanova ana kibarua kigumu cha kufanya katika kuimarisha safu yake ya mabeki kabla ya mechi yao ya nyumbani dhidi ya Valencia mwishoni mwa wiki hii baada ya makosa ya Gerard Pique na Javier Mascherano kuwapa mahasimu wao Real Madrid taji la Super Cup la Hispania.


Kikosi cha kocha Jose Mourinho kilifunga mara mbili ndani ya dakika 19 za kwanza kwenye Uwanja wa Bernabeu juzi, kikitumia makosa ya mabeki wote hao wa kati kuibuka na ushindi wa 2-1 na kumpa Vilanova kipigo chake cha kwanza tangu amrithi Pep Guardiola.


Katika mechi yao ya kwanza wiki iliyopita, alikuwa ni kipa Victor Valdes aliyefanya 'madudu'
yaliyomruhusu Angel Di Maria kuipa goli Real ambalo mwishowe likawapa taji lao la kwanza msimu huu kwa faida ya sheria ya goli la ugenini kufuatia matokeo ya jumla ya sare ya 4-4.


Barca, wanaowakaribisha Valencia Jumapili (saa 4:30 usiku), wanaongoza katika msimamo wa La Liga, Ligi Kuu ya Hispania baada ya kushinda mechi zote mbili walizocheza lakini wameonyesha kutetereka katika eneo la ulinzi katika mechi hizo za ufunguzi wa msimu.


"Kuna mambo tunayopaswa kurekebisha," Vilanova aliwaambia waandishi wa habari baada ya kipigo hicho, akichagua kuangalia zaidi namna timu yake ilivyocheza baada ya kutanguliwa kwa magoli hayo na kutolewa Adriano katika dakika ya 29, ambapo walitulia na kufunga goli lao kupitia 'fri-kiki' kali ya Lionel Messi muda mfupi kabla ya mapumziko.


Pique ambaye ni beki wa Barca na timu ya taifa ya Hispania aliwaambia waandishi wa habari: "Tulipaswa kucheza vizuri zaidi mwanzoni mwa mechi, lakini tunastahili pongezi kucheza hapa kwa namna tuliyoonyesha huku tukiwa na watu 10."


"Tulianza mechi vibaya na makosa yale mawili yalitugharimu," Xavi aliiambia televisheni ya Hispania.
"Lakini pamoja na mabao yao mawili huku sisi tukiwa 10, tulijibu mapigo na kupata nafasi mbili safi ambazo zingeweza hata kutupatia kombe," aliongeza.


"Tumepoteza kombe hili lakini makombe mengine muhimu zaidi bado yapo kwa ajili yetu."

MKOSI WA KWANZA
Barcelona wanakabiliwa pia na tishio la kumkosa beki wa kulia, Dani Alves, ambaye alilazimika kujiondoa katika kikosi kilichocheza juzi dakika chache kabla ya mechi kuanza baada ya kupatwa na maumivu ya misuli wakati wakifanya mazoezi mepesi.


Wakati Vilanova akikabiliwa na tatizo hilo la kwanza msimu huu, Mourinho ameonekana kupata ahueni kwa kukabiliana vyema na changamoto zilizokuwa zikimkabili.


Real walishindwa kuambulia ushindi katika mechi zao tatu za mwanzo wa msimu, wakishikiliwa kwa sare ya nyumbani ya 1-1 dhidi ya Valencia, wakalala katika mechi ya kwanza ya Super Cup kwa mabao 3-2 mjini Barcelona na baadaye wakapata kipigo kisichotarajiwa cha mabao 2-1 katika mechi ya ugenini ya La Liga dhidi ya Getafe.


Mourinho aliponda kiwango kibovu cha wachezaji wake baada ya kuchapwa na Getafe na alionekana kupata matunda ya kasoro walizojirekebisha wakati waliposhinda nyumbani kwao dhidi ya Barca kwa mara ya kwanza baada ya mechi saba ndani ya miaka minne.


"Hii ndio Real Madrid ambayo wote tunataka kuiona," beki wa Real na timu ya taifa ya Hispania, Alvaro Arbeloa aliwaambia waandishi wa habari.


"Sisi ni wa kwanza kukiri kwamba hatukucheza vizuri dhidi ya Valencia na Getafe. Kocha alikuwa sahihi. Hii ndio picha tunayotaka kuionyesha."


Kipa na nahodha wa Real Madrid, Iker Casillas alisema: "Kwenye Uwanja wa Nou Camp walikuwa na nafasi ya kufunga goli la nne lakini wakakosa na kilichofuata ni sisi kupata goli lililoendelea kutupa nafasi."


"Tulitawala kipindi cha kwanza na mechi nzima kwa ujumla, ingawa tulikuwa na wakati mgumu kuelekea mwishoni mwa mechi," aliongeza.


"Tulikuwa na kiwango kibovu na hivyo tulikuwa na deni kwa mashabiki. Hatukuuanza msimu vizuri, lakini kuna siku mnakuwa na bahati na siku nyingine mnakosa."


Katika mechi 221 walizokutana hadi sasa, Real Madrid wanaongoza dhidi ya Barca kwa kushinda mechi 88-87.


Mourinho hakuzungumza baada ya ushindi wao uliowapa taji la Super Cup. Real watacheza nyumbani Jumapili katika mechi yao ya La Liga dhidi ya Granada (saa 2:50 usiku).

REUTERS

No comments:

Post a Comment