Thursday, August 30, 2012

NI BENDI YA MAPACHA WATATU, AMA KIKUNDI CHA MATARUMBETA?


Bila ya shaka nawe imewahi kukutokea. Unaweza kwenda mahala pako pa kutafutia riziki kisha ukajikuta na wenzako kadhaa mmevaa sare bila ya kupanga. Au umeingia hotelini/baa na kukuta nguo zako ulizovaa ndio sare za wahudumu. Ofisini The Guardian huwa ni burudani sana pale watu wanapojikuta wamevaa sare ilhali hamna sare ya ofisi. Utani huwa mwingi na mara zote waliolingana rangi za mavazi huambiwa wameanzisha bendi. Watu hufurahi sana yanapotajwa majina ya bendi mbalimbali. Leo waandishi hawa wa habari, pichani kutoka kushoto Raphael Kibiriti, Abdul Mitumba na Sabato Kasika waliitwa bendi ya "Mapacha Watatu" baada ya kujikuta bila ya kutarajia wamevaa sare huku tena bila ya kutarajia kujikuta wamekaa pamoja. Ilikuwa raha sana. Ni kazi na furaha....

No comments:

Post a Comment