Monday, August 27, 2012

REAL MADRID WAMALIZANA NA TOTTENHAM LEO USAJILI WA LUKA MODRIC... WAMNG'OA KWA EURO MILIONI 42 (SH. BILIONI 80)... AKIFUZU VIPIMO VYA AFYA KUSAINISHWA MKATABA MIAKA MITANO..!

Luka Modric akiwa kazini
Bao...! Luka Modric akishangilia baada ya kuifungia goli Tottenham
MADRID, Hispania
Real Madrid wamekubali leo kumsajili kiungo - mchezeshaji wa Croatia, Luka Modric kutoka klabu ya Tottenham Hotspur kwa mkataba wa miaka mitano, mabingwa hao wa La Liga, Ligi Kuu ya Hispania wamesema leo.

"Real Madrid CF na Tottenham Hotspur wamefikia makubaliano ya uhamisho wa mchezaji Luka Modric, ambaye atabaki na klabu hii kwa misimu mitano ijayo," Real wamesema kupitia tovuti yao (www.realmadrid.com).

Tottenham, ambao pia wamethibitisha makubaliano hayo kupitia tovuti yao (www.tottenhamhotspur.com) wamesema kilichobaki sasa ni kwa Modric kufuzu vipimo vya afya na pia makubaliano ya kirafiki baina ya klabu hizo mbili ambayo yatazifanya zishirikiane katika "masuala ya wachezaji, ufundishaji na biashara".

Ingawa hakuna klabu yoyote kati ya hizo iliyoeleza dau la uhamisho wa kiungo huyo, vyombo vya habari vya Hispania vimeripoti kuwa Real wamemtwaa kwa euro milioni 35, pamoja na ziada ya euro milioni 7 ikiwa kiungo huyo mwenye miaka 26 ataipa mafanikio, hivyo jumla ya gharama za uhamisho kufikia euro milioni 42 (Sh. bilioni 80).

Modric alitua Tottenham akitokea Dinamo Zagreb mwaka 2008.

No comments:

Post a Comment