Wednesday, August 1, 2012

RAIS CWT AFICHUA NAMNA SERIKALI ILIVYOWAFYEKA MISHAHARA WALIMU NA SIO KUWAONGEZA

Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Kawawa jijini Dar es Salaam wakionekana barabarani baada ya walimu wao kugoma. 
Rais wa CWT, Gratian Mukoba (kushoto)
Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Gratian Mukoba, amesema kuwa madai ya Serikali kwamba wamewaongeza walimu mshahara kwa asilimia 14 ni ya kinadharia zaidi kwani ukweli ni kwamba wamewapunguzia mshara kwa asilimia 5.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Mukoba alisema kuwa kauli ya serikali iliyorejewa na Waizir Kawambwa jana ni kinyume na uhalisia wa maisha, akifafanua kuwa hivi sasa, serikali yenyewe inakiri kupitia takwimu zake za kiuchumi kuwa mfumuko wa bei sasa umefikia asilimia 19, hivyo kudai kwamba wamewaongezea mshahara kwa asilimia 14 ni nadharia tu kwani kimahesabu, hiyo ni sawa na punguzo la asilimia tano katika kiasi wanachopata sasa.

"Walimu huwa tunafundisha hesabau za hasi na chanya... kama wameongeza asilimia 14 bila kutushirikisha, halafu mfumuko wa bei wa sasa ukaendelea kuwa asilimia 19, maana yake kilichotokea ni sawa na kulipa Sh. 14 katika deni la Sh. 19... hapo litabaki deni la Sh. 5.... kwahiyo kiuhalisia ni kwamba mshahara wa walimu umepunguzwa kwa asilimia tano," alisema Mukoba.

CWT imetangaza mgomo wa walimu katika nchi nzima kuishinikiza serikali itekeleze madai yao ya kuongezewa mshahara kwa asilimia 100, posho kwa asilimia 50 na 55 (kwa walimu wa sayansi) na pia kuwalipa posho ya mazingira magumu ya asilimia 30 ya mshahara.

Serikali imepinga mgomo huo kortini na kesho shauri lao linatarajiwa kutolewa hukumu na hakimu Sophy Wambura wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi Kanda ya Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment