Wednesday, August 1, 2012

RAIS KIKWETE ASISITIZA: SERIKALI HAIHUSIKI KIPIGO CHA DK. ULIMBOKA

Rais Jakaya Kikwete

Dk. Ulimboka akiwa hospitalini
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Kikwete, amesisitiza jioni hii kwamba serikali haikuhusika na wala haina sababu yoyote ya kumdhuru kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari, Dk. Steven Ulimboka.

Rais Kikwete ameyasema hayo jioni hii jijini Dar es Salaam wakati akiendelea kuzungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini.

"Hizi ni stori tu... nitamshangaa huyo mtu wa serikali kwenda kumpiga Dk. Ulimboka, kwa sababu ipi?" amesema.

Kikwete alitoa ufafanuzi huo kufuatia swali aliloulizwa juu ya uvumi ulioenea kuwa serikali,  kupitia Idara ya Usalama wa Taifa, ndiyo iliyohusika katika kumteka Dk. Ulimboka na kumtesa kabla ya kumtupa kwenye msitu wa Mabwepande jijini Dar es Salaam.

Dk. Ulimboka alikuwa mstari wa mbele wakati wa mgomo wa madaktari nchini na hivi sasa anaendelea kutibiwa nchini Afrika Kusini.Hadi sasa, Rais Kikwete anaendelea kujibu maswali ya wahariri.

No comments:

Post a Comment