Wednesday, August 22, 2012

PEPE ATOLEWA HOSPITALI... KUIKOSA 'EL CLASICO' YA REAL MADRID DHIDI YA BARCELONA ITAKAYOPIGWA KESHO SAA 5:30 USIKU KWA SAA ZA KIBONGO...!

Pepe akisaidiwa kutoka uwanjani baada ya kusumbuliwa na maumivu ya majeraha ya kichwa katika mechi yao ya Jumapili iliyopita dhidi ya Valencia kwenye Uwanaj wa Santiago Bernabeu.  
MADRID, Hispania
BEKI wa Real Madrid, Pepe amesema kuwa sasa anajisikia vizuri baada ya kutolewa hospitali jana na kuwashukuru mashabiki kutokana na sapoti waliyompa.

Pepe alifanyiwa vipimo vya 'scan' baada ya kuumia kichwani kufuatia kugongana na kipa wake Iker Casillas wakati wa mechi yao ya ufunguzi wa La Liga, Ligi Kuu ya Hispania dhidi ya Valencia iliyochezwa Jumapili na kumalizika kwa sare ya 1-1.

Beki huyo amesema: "Nataka niwashukuru wote kwa salamu nyingi mlizonitumia za kunisapoti tangu nilipoumia. Nimefarijika na namna nilivyokuwa nikipewa moyo tangu Jumapili, hasa na mashabiki wa Real Madrid fans, kwakweli nilipata nguvu. Muda si mrefu nitapona kabisa na kuendelea kuipigania klabu yetu.

"Sapoti niliyoendelea kuipata kutoka kwa wachezaji wenzangu, makocha, viongozi na wafanyakazi wote wa klabu imekuwa kubwa sana. Nataka nitoe shukrani za pekee kwa madaktari wa klabu yetu, ambao muda wote wamekuwa na bado wako pembeni yangu katika muda wote.

"Nataka pia kuwashukuru wachezaji wote kutoka klabu nyingine ambao wamekuwa wakiguswa kwa namna mbalimbali na kunitakia afya njema. Hizi ni ishara njema ambazo kamwe hazitasahaulika. Shukrani kwa kila mmoja."

Habari mbaya kwa mashabiki wa Real Madrid ni kwamba, licha ya Pepe kupata nafuu na kutolewa hospitali, hatakuwamo katika kikosi kitakachocheza kesho dhidi ya Barcelona katika mechi yao ya kwanza ya kuwania taji la Super Cup itakayochezwa kwenye Uwanja wa Nou Camp kuanzia saa 5:30 usiku kwa saa za Tanzania!

No comments:

Post a Comment