Wednesday, August 22, 2012

ALEX SONG: NILIKUBALI OFA YA BARCELONA KIRAHISI MNO KWA SABABU WANANGU WAMEKUWA WAKINISUMBUA KUTAKA KUMUONA LIONEL MESSI 'LIVE'... TENA WOTE WANAJIITA MESSI, MESSI...!

Hapa hata nikisotea benchi msimu mzima poa tu... Song (kushoto) akipiga makofi wakati wa utambulisho wa wachezaji wa Barcelona kwenye Uwanja wa Nou Camp jana. Wengine ni Cesc Fabregas (katikati) na Jordi Alba.

Karibu kijana... hapa utapata vyote -- makombe na mkwanja! Rais wa Barca, Sandro Rosell akimkaribisha Song wakati akijiandaa kwa vipimo vya afya juzi.

Nishike na mie... mashabiki wa Barca wakigombea kushikana mikono na Song mjini Barcelona jana..

'Jini' Messi likimuacha kwa kasi beki Enaut Zubireka wa Real Sociedad wakati wa mechi yao ya La Liga, Ligi Kuu ya Hispania Jumapili. Katika mechi hii, Messi alitupia mabao mawili wakati Barca ikiua 5-1... vitu kama hivi nd'o huwachanganya watoto wa Song. 

Messi hazuiliki bila kumfanyia mbinu chafu kama hii... Song akihaha kumdhibiti Messi kwa kumpiga kwanja wakati wa mechi mojawapo ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kati ya klabu yake ya zamani ya Arsenal na Barcelona iliyopigwa Februari, 2011.
BARCELONA, Hispania
Kiungo mpya wa Barcelona, Alex Song amesema kuwa alikubali kirahisi kujiunga na klabu yake ya sasa mara tu alipofuatwa kwa sababu wanawe wa kiume siku zote walikuwa wakimsumbua kutaka nafasi ya kumuona 'live' Lionel Messi.

Song amefichua hayo leo ikiwa ni siku moja tu baada ya kutambulishwa kwa mashabiki wa Barca jana kufuatia kukamilika kwa uhamisho wake akitokea klabu ya Arsenal uliogharimu ada ya paundi za England milioni 15 (Sh. bilioni 37).

“Kwa haraka kabisa nilikubali kwa kusema ndiyo. Nimefurahi sana kuwa hapa Barcelona. Ni siku ya aina yake kwangu na pia kwa familia yangu. Kupata nafasi ya kuichezea klabu bora zaidi duniani huja mara moja tu katika maisha,” amesema Song.

“Najua Barça wameshatwaa kila taji, lakini naamini kwamba hii ni timu inayotaka kuendelea kushinda kila kitu. Nitajitahidi kufanya kila ninaloweza kuhakikisha kwamba nami nasaidia kuendeleza lengo hilo.

“Nina watoto wawili wa kiume ambao wanachizika na Messi. Wakati wakicheza kwenye bustani hujifanya kuwa wao ni Messi. Yeye (Messi) ana kipaji cha ajabu, ndiye mwanasoka bora kuliko wote."

No comments:

Post a Comment