Wednesday, August 22, 2012

HATIMAYE EMMANUEL ADEBAYOR ATUA JUMLA TOTTENHAM AKITOKEA MANCHESTER CITY

Emmanuel Adebayor
LONDON, England
EMMANUEL Adebayor hatimaye amekamilisha uhamisho wake kutoka kwa mabingwa wa Ligi Kuu ya England, klabu ya Manchester City kwenda Tottenham, klabu yake imethibitisha.

Straika huyo wa kimataifa wa Togo mwenye miaka 28, ambaye aliwahi kuichezea kwa mkopo Real Madrid kabla ya kutua kwa mkopo pia Tottenham msimu wa 2011-12, alikuwa wa kwanza kutoa taarifa hiyo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa tweeter, akiwaahidi mashabiki kwa kuwaambia kuwa ana njaa ya kufunga mabao mengi zaidi kwa ajili ya klabu yake mpya.

"Nimerudi!!!! Nakuja Tottenham!! Nina njaa ya mabao...jiandaeni," aliandika katika ukurasa wake rasmi wa Twitter.

Baada ya kufunga mabao 18 katika mechi 37 alizoichezea Tottenham msimu uliopita, kocha mpyaAndre Villas-Boas alipania kuendelea kuwa na straika huyo kwenye kikosi chake, ambacho alijiunga nacho huku kikiwa na Jermain Defoe tu aliyekuwa mzoefu katika nafasi hiyo.

Katika mahojiano yake na tovuti rasmi ya Tottenham, Adebayor alizungumzia furaha yake ya kusajiliwa na klabu iliyomaliza katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi kuu ya England msimu uliopita, akieleza pia dhamira yake ya kuendelea kufanya vizuri klabuni hapo.

"Nimefurahi kusajiliwa Tottenham kwa mkataba wa kudumu baada ya mwishowe kukubali kuachana kwangu na Manchester City," alisema.

"Inaweza ikawa imechukua muda mrefu kukamilisha hili kuliko ilivyotarajiwa, lakini nimefurahi kurudi Tottenham Hotspur.  Kwakweli nilikuwa na kipindi kizuri wakati nikiwa hapa msimu uliopita na ninatumai kwamba tunaweza kufanya mambo makubwa tukiwa tena pamoja."

No comments:

Post a Comment