Monday, August 27, 2012

NYOTA KUTOKA JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO KUZIBA NAFASI YA GEORGE ODHIAMBO 'BLACKBERY' ALIYEFUNGASHIWA VIRAGO AZAM LEO ..!

Klabu ya Azam imetangaza kuwa sasa iko mbioni kumsajili nyota mmoja wa kimataifa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ili kuziba nafasi iliyochwa wazi na Mkenya George Odhiambo 'Blackbery' aliyetimuliwa leo kutokana na utovu wa nidhamu.

Afisa Habari wa Azam, Jafari Iddi, amesema kuwa klabu yao kamwe haiwezi kuvumilia vitendo vya utovu wa nidhamu na ndiyo maana wakaachana na 'Blackbery' na kuamua kusaka nyota mwingine wa kigeni atakayechukua nafasi yake.

"Azam inajali nidhamu na hivyo haikuweza kumvumilia Blackbery... alikuwa hajaripoti mazoezini kwa siku nne na tena bila ya kutoa taarifa zozote. Hivyo tumeachana naye kwavile amevunja mkataba yeye mwenyewe kutokana na kitendo chake hicho," amesema Iddi.

Akaongeza kuwa wanaendelea kumfanyia majaribio nyota mmoja kutoka Kongo na kwamba, wakiridhika naye watamsajili na kutangaza jina lake kwani tarehe ya mwisho kwa usajili wa wachezaji wa kigeni (Septemba 10) bado haijafikiwa.

No comments:

Post a Comment