Thursday, August 30, 2012

MAKUNDI YA LIGI YA KLABU BINGWA ULAYA 2012-13... MAN UTD WANACHEEEKA, REAL MADRID KUNDI LA KIFO, ARSENAL SI MBAYA SANA, CHELSEA KUWAKABILI JUVE, INIESTA MWANASOKA BORA UEFA AWAPIKU MESSI, RONALDO

Straika Muargentina, Lionel Messi (kushoto) akimpongeza kiungo wa FC Barcelona, Andres Inesta (kulia) wa Hispania baada ya kushinda tuzo ya Mchezaji Bora wa UEFA 2012 wakati Mreno Cristiano Ronaldo (kushoto) akiangalia pembeni wakati wa hafla ya upangaji wa makundi ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya 2012/2013 kwenye ukumbi wa Grimaldi Forum wa Monte Carlo mjini Monaco leo Agosti 30, 2012. Picha: REUTERS
Kiungo wa FC Barcelona, Andres Iniesta (kushoto) wa Hispania akipokea tuzo ya Mchezaji Bora wa UEFA 2012 kutoka kwa Rais wa UEFA, Michel Platini wakati wa hafla ya upangaji wa makundi ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya 2012/2013 kwenye ukumbi wa Grimaldi Forum wa Monte Carlo mjini Monaco leo Agosti 30, 2012. Picha: REUTERS

Kiungo wa FC Barcelona, Andres Iniesta wa Hispania akishikilia tuzo yake ya Mchezaji Bora wa UEFA 2012 baada ya kutuzwa wakati wa hafla ya upangaji wa makundi ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya 2012/2013 kwenye ukumbi wa Grimaldi Forum wa Monte Carlo mjini Monaco leo Agosti 30, 2012. Picha: REUTERS
Washindi watatu wa kwanza waliokuwa wakiwania tuzo ya Mwanasoka Bora wa UEFA 2012 kutoka kushoto Mhispania Andres Iniesta, Muargentina Lionel Messi na Mreno Cristiano Ronaldo wakiwa katika hafla ya upangaji wa makundi ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya 2012/2013 kwenye ukumbi wa Grimaldi Forum wa Monte Carlo mjini Monaco leo Agosti 30, 2012. Picha: REUTERS

Kiungo wa FC Barcelona, Andres Iniesta wa Hispania akishikilia tuzo yake ya Mchezaji Bora wa UEFA 2012 baada ya kutuzwa wakati wa hafla ya upangaji wa makundi ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya 2012/2013 kwenye ukumbi wa Grimaldi Forum wa Monte Carlo mjini Monaco leo Agosti 30, 2012. Picha: REUTERS
Washindi watatu wa kwanza waliokuwa wakiwania tuzo ya Mwanasoka Bora wa UEFA 2012 kutoka kushoto Mhispania Andres Iniesta, Muargentina Lionel Messi na Mreno Cristiano Ronaldo wakipiga makofi wakati wa hafla ya upangaji wa makundi ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya 2012/2013 kwenye ukumbi wa Grimaldi Forum wa Monte Carlo mjini Monaco leo Agosti 30, 2012. Picha: REUTERS

MONACO, Ufaransa
MABINGWA wa Ulaya Chelsea watakabiliana na mabingwa wa zamani Juventus, Shakhtar Donetsk ya Ukraine na timu inayoshiriki kwa mara ya kwanza kutoka Denmark, FC Nordsjaelland katikahatua ya makundi ya msimu huu kufuatia upangaji wa makundi uliofanyika leo.

Mfululizo wa mechi ngumu unatarajiwa katika Kundi D baada ya mabingwa mara tisa wa Ulaya, Real Madrid kupangwa dhidi ya mabingwa wa England, Manchester City, mabingwa wa Uholanzi, Ajax Amsterdam na mabingwa wa Ujerumani, Borussia Dortmund.

Bayern Munich, ambao walifungwa katika mechi ya fainali ya Ligi ya Klabu Bingwa msimu uliopita na ambao walimaliza wa pili nyuma ya Dortmund katika Bundesliga, watawakabili Valencia, Lille na BATE Borisov wa Belarus katika Kundi F.

Barcelona, waliokuwa wakipewa nafasi kubwa msimu uliopita hadi walipotolewa na Chelsea katika nusu fainali, watawakabili mahasimu wao wa zamani Benfica, Spartak Moscow na Celtic.

Manchester United wamepangwa pamoja na Braga, Galatasaray na CFR Cluj katika Kundi H, wakati Arsenal watawakabili Schalke 04, Olympiakos Piraeus na Montpellier HSC ya Ufaransa aliyotokea mshambuliaji wao mpya Olivier Giroud. 

Michuano hiyo itaanza Septemba 18-19 na fainali itafanyika kwenye Uwanja wa Wembley Mei 25.

Makundi ya Ligi ya Klabu Bingwa ya Ulaya yaliyopangwa leo mjini Monaco:
   
    Kundi A
    Porto
    Dynamo Kiev
    Paris St Germain
    Dinamo Zagreb
   
    Kundi B
    Arsenal
    Schalke 04
    Olympiakos Piraeus
    Montpellier HSC 
   
    Kundi C
    AC Milan
    Zenit St Petersburg  
    Anderlecht
    Malaga
   
    Kundi D
    Real Madrid
    Manchester City
    Ajax Amsterdam
    Borussia Dortmund
   
    Kundi E
    Chelsea
    Shakhtar Donetsk
    Juventus
    Nordsjaelland
   
    Kundi F
    Bayern Munich
    Valencia
    Lille
    BATE Borisov
   
    Kundi G
    Barcelona
    Benfica
    Spartak Moscow 
    Celtic
   
    Kundi H
    Manchester United
    Braga
    Galatasaray
    CFR Cluj
--------------------------------------------------------------------------------

No comments:

Post a Comment