Tuesday, August 28, 2012

NANI AJADILI KUJIUNGA NA ZENIT ST PETERSBURG

Nani

ZENIT St Petersburg wametuma maombi ya kutaka kumsajili winga wa Manchester United, Nani.

Gazeti la Daily Mail limesema kuwa Zenit wako tayari kutoa paundi milioni 25 kwa ajili ya kumsajili Nani, ambaye hajaafiki mktaba mpya Old Trafford.


Wawakilishi wa mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Ureno walikutana na wawakilishi wa Zenit mjini Amsterdam juzi Jumatatu kwa ajili ya mazungumzo ya kufanikisha dili hilo.


"Habari kuhusu Nani ni kweli," kocha wa Zenit, Luciano Spalletti alisema.


"Kila kitu kinategemea ni kiasi gani mchezaji atatugharimu kwa sababu hatutalipa fedha nyingi za ziada."

No comments:

Post a Comment