Friday, August 10, 2012

MKENYA DAVID RUDISHA AVUNJA REKODI YA DUNIA MBIO MITA 800

Mkenya David Rudisha akiwa mbele ya bango linaloonyesha rekodi yake mpya ya dunia aliyoweka

LONDON, Uingereza
DAVID Rudisha alikuwa mwanariadha wa kwanza kuweka rekodi mpya ya dunia katika Michezo ya Olimpiki ya London 2012 wakati aliposhinda medali ya dhahabu ya mika 800.

Mkenya huyo mwenye umri wa miaka 23 alitwaa ushindi katika Michezo ya Olimpiki ambayo alikuwa akishiriki kwa mara ya kwanza na kuwa mtu wa kwanza kukimbia kwa muda wa ndani ya dakika moja na sekunde 41, akiwa ametumia muda wa dakika 1:40.91.

Mwanariadha wa Botswana mwenye umri wa miaka 18, Nijel Amos alichukua medali ya fedha, huku yosso wa Kenya, Timothy Kitum, akiondoka na ya fedha.

Muingereza Andrew Osagie aliishia kushika nafasi ya nane lakini bado aliweka rekodi yake binafsi bora ya muda wa dakika 1:43.77.

Bingwa mtetezi wa dunia Rudisha aliongoza kutokea mwanzo, na kuwaacha wenzake kwa umbali wa muda wa sekunde 49.28 na akawaacha mbali zaidi walipokaribia mita 100 na kuipiku rekodi yake mwenyewe ya dunia.

Rudisha aliiambia BBC Sport: "Wow! Nina furaha sana. Hiki ni kipindi ambacho nilikuwa nikikisubiri kwa muda mrefu sana. Kuwepo hapa na kuvunja rekodi ya dunia ni kama ndoto.

"Nilijiandaa vyema na sikuwa na shaka kwamba nitashinda. Leo hali ya hewa ilikuwa nzuri na nikaamua kufanya kweli."

Lakini Rudisha anasema angeweza kukimbia kwa kasi zaidi.

Alisema: "Baada ya kukimbia raundi mbili kabla ya kumaliza nilianza kujisikia nimechoka kidogo. Nilimweleza daktari wangu jana kuwa nilikuwa najisikia vibaya baada ya kukimbia nusu fainali, hivyo kama nitaboresha hilo bado ninayo nafasi ya kuweka rekodi bora zaidi."

No comments:

Post a Comment