Saturday, August 4, 2012

MAN UTD KUWAPIKU ARSENAL KWA SAHIN

Nuri Sahin

MANCHESTER United wanatishia mipango ya Arsenal ya kutaka kumsajili kiungo wa Real Madrid, Nuri Sahin.

Gazeti la Marca limesema Man United imejumuika katika mbio za kutaka kumsajili kiungo huyo "jembe" ambaye hana namba katika kikosi cha Jose Mourinho.

Nyota huyo wa Uturuki, tayari ameambiwa na Mourinho kwamba anaweza kwenda kwenye klabu anayotaka.

Arsenal na Tottenham zinamhitaji kwa mkopo lakini kocha wa United, Sir Alex Ferguson ameripotiwa kutaka kumsajili jumla.

No comments:

Post a Comment