Saturday, August 4, 2012

CAZORLA AMVUTIA RVP KUBAKI ARSENAL


ROBIN van Persie anaaminika kwamba ameanza kulegeza msimamo wake na huenda akabaki Arsenal.

Gazeti la Daily Star limesema kuwa Mholanzi huyo amevutiwa sana na juhudi zinazofanywa kuimarisha kikosi cha Arsenal, baada ya jana kutua kwa kiungo wa kimataifa wa Hispania, Santiago Cazorla.

Winga huyo, ambaye pia hucheza kama kiungo wa kati, anaaminika kugharimu paundi milioni 12.65 tu, huku Arsenal ikitumia udhaifu uliopo Malaga wa matatizo ya kifedha kumsajili kiulaini.

Carzola alijiunga na Arsenal jana na anatarajiwa kuungana na wenzake kwenye kambi ya mazoezi nchini Ujerumani wiki ijayo, huku vijana wa Arsene Wenger wakicheza mechi ya kirafiki dhidi ya FC Cologne wiki ijayo.

Atajumuika safarini pamoja na Van Persie, huku klabu ikizidi kupata matuamini kwamba atashawishika kubadili msimamo wake wa kutaka kuhama.

Inafahamika kwamba nahodha huyo wa Gunners, bado moyo wake umejaa Arsenal, na hajafurahishwa na namna klabu zinazomuwinda za Manchester City, ­Manchester United na ­Juventus zinafanya juhudi ndogo kumpata.

No comments:

Post a Comment