Wednesday, August 22, 2012

MAN U WAMCHENJIA LUIS NANI... OMBI LAKE MSHAHARA MPYA KUTOSWA

MANCHESTER, England
Kocha wa Manchester United, Sir Alex Ferguson yuko tayari kuachana na Nani baada ya kipigo walichopata juzi katika mechi yao ya ufunguzi wa Ligi Kuu ya England dhidi ya Everton.

Gazeti la The Sun limesema leo kwamba straika huyo wa kimataifa  wa Ureno 'ataonja joto ya jiwe' kutokana na kiwango cha chini alichoonyesha katika mechi ya juzi waliyolala ugenini kwa bao 1-0.

Imeelezwa zaidi kuwa Nani anaweza pia kusahau kabisa kuhusu ndoto za mazungumzo ya mkataba mpya yatakayomfanya aongezewe mshahara wake -- au ajiandae kuuzwa kwa bei poa.

Chanzo kutoka ndani ya Man U kimesema: “Klabu haidhani kwamba kiwango chake kuelekea mwishoni mwa msimu uliopita kinampa nafasi thabiti ya mazungumzo juu ya mkataba mpya. Hata hivyo, kiwango alichoonyesha Jumatatu kilikuwa na afadhali zaidi kwake.”

Ashley Young anaandaliwa kutwaa nafasi ya Nani katika mechi yao ya Jumamosi dhidi ya Fulham.

Nani, 25, amekatishwa tamaa na kuvunjika kwa mazungumzo kuhusu mkataba wake mpya utakaombakiza Man U kwa miaka mingine minne.

Chanzo ndani ya Man U kimeongeza: “Kulikuwa na mpango wa kumsainisha mkataba mpya wa miaka minne.

“Lakini mshahara wa awali alioutaka Nani ulikuwa wa juu mno. Hivi sasa Man U wako tayari kusitisha mpango huo hadi kipindi kijacho cha usajili wa majira ya kiangazi, labda abadili uamuzi wake wa kutaka dau kubwa. Lakini hawawezi kumuuza kwa sasa labda wakipata ofa nono.”

No comments:

Post a Comment