Thursday, August 23, 2012

MADEMU WAMYUMBISHA KIWANGO RONALDO

Ronaldo akijiachia na demu wake Irina Shayk kwenye boti ya kifahari wakati wa likizo ya kuelekea msimu huu.
Straika wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo akijiuliza baada ya kupoteza nafasi ya kufunga wakati wa mechi yao ya ufunguzi wa Ligi Kuu ya Hispania (La Liga) dhidi ya Valencia kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid Agosti 19, 2012. Ronaldo "alipotea" katika mechi hiyo ambayo Real walitoka 1-1, huku goli la Real likifungwa na Higuain. Picha: REUTERS

Ronaldo akijicheza na demu wake Irina Shayk wakati wa likizo ya kuelekea msimu huu.
Ronaldo akila denda na demu wake Irina Shayk wakati akiwa mapumzikoni. Hii nayo vipi, sio hatari kwa soka lake? 
Ronaldo akiponda maraha na demu wake Irina Shayk.

KUNA maswali mengi kuhusu hali ya sasa ya kiakili ya straika wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo.

Gazeti la El Mundo Deportivo la Hispania limesema kuwa Ronaldo bado hajasahau machungu ya kushindwa kwa Ureno katika fainali za Mataifa ya Ulaya (Euro) 2012, jambo lililochangia kuwa na mchango katika mwanzo wa msimu. Inadaiwa kwamba, tayari anajiona ameshachoka wakati msimu ndio kwanza una wiki moja tu tangu uanze.

Nyongeza ya matatizo ya Ronaldo yanadaiwa kuwa ni kitendawili cha mahusiano yake ya kimapenzi yanayomhusisha demu wake wa miaka mingi, Irina Shayk na Mtangazaji wa televisheni ya Ureno, Rita Pereira.

Inadaiwa kwamba mama wa Ronaldo, Dolores, hajawahi kumkubali Irina na angependa kumuona Cristiano akiwa na Rita.

Ronaldo amepata kuwa na mahusiano na vimwana kibao akiwamo Paris Hilton.

No comments:

Post a Comment