Thursday, August 23, 2012

KOCHA LIVERPOOL: LAZIMA NIWE KICHAA ILI NIKUBALI SASA KUMUUZA ANDY CARROL

Andy Carroll

Brendan Rodgers... kufikiria sasa kumuuza Andy Carroll ni uwendawazimu!
LIVERPOOL, England
Andy Carroll ameshindwa kuonyesha kiwango kinachoendana na thamani ya dau lililotumika kumhamisha kutoka Newcastle United kwenda Liverpool, na licha ya kuanzia benchi katika mechi ya ufunguzi wa msimu mpya wa Ligi Kuu ya England, kocha Brendan Rodgers amesema atakuwa kichaa kama atakubali kumuachia straika huyo.

Rodgers, aliyetwaa nafasi ya kuinoa Liverpool baada ya kuondoka kwa Kenny Dalglish mwezi Juni, alitupilia mbali ombi la Newcastle kumrejesha klabuni kwao straika huyo mwenye nguvu kwa mkopo na kusema kuwa kamwe hawezi kupunguza zaidi safu yake ya ushambuliaji ambayo hadi sasa ina wachezaji pungufu huku akijua wazi kwamba dirisha la usajili wa majira ya kiangazi linakaribia kufungwa.

"Kwa uchache nahitaji mastraika . Mara dirisha litakapofungwa, itamaanisha kuwa hakuna nafasi ya kuongeza mwingine hadi Januari. Ninao (Luis) Suarez, Fabio Borini na Andy Carroll," amewaambia waandishi wa habari.

"Nitalazimika kuwa kichaa hivi sasa ili nifikirie kumuachia Carroll aondoke, labda niwe na mbinu mbadala kwa jili ya jambo hilo."

Carroll alionyesha kidogo kiwango kuelekea mwishoni mwa msimu uliopita na kupata nafasi ya kuwemo katika kikosi cha England kilichoshiriki fainali za Euro 2012, lakini alibaki akisotea benchi katika ushindi wa  Liverpool wa mabao 3-0 katika mechi yao ya ufunguzi waliyofungwa na West Bromwich Albion.

West Ham United pia wanamfukuzia straika huyo mwenye miaka 23 lakini baada ya kuachiwa kwa washambuliaji Dirk Kuyt na Craig Bellamy, Rodgers amejikuta katika wakati mgumu.

"Kwa hakika hakuna nafasi kabisa (ya mpango wa kumuachia kwa mkopo) -- na hasa kwa Newcastle," kocha huyo wa zamani wa Swansea City alisema.

"Newcastle walipata paundi milioni 35 (Sh. bilioni 87) kwa kumuuza straika huyu mwaka jana. Kitendo cha kufikiria tu kumtaka tena kwa mkopo ni mzaha mkubwa."

No comments:

Post a Comment