Tuesday, August 28, 2012

LUKA MODRIC: REAL MADRID ND'O TIMU BORA


Luka Modric akiwa na Rais wa Real Madrid, Florentino Perez

Luka Modric akisalimia mashabiki Real Madrid

Luka Modric

Luka Modric

Luka Modric alipokuwa akijiandaa ndani ya vyumba vya kuvalia kwenye Uwanja wa Bernabeu 
Luka Modric akionyesha vitu vyake kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu wakati wa utambulisho wake jana. 
MADRID, Hispania
KIUNGO wa zamani wa Tottenham, Luka Modric ameelezea furaha aliyonayo baada ya kukamilisha uhamisho wake wa kujiunga na Real Madrid jana.


Alisema: "Ndio nina furaha sana kufanikiwa kuja hapa katika timu bora yenye wachezaji bora duniani, na kocha bora duniani… siwezi kuwa na kingine cha kuomba. Nina furaha kubwa, kubwa sana.


"Nilikuwa nasubiri kila dakika ili jambo litokee… hatimaye likatokea jana (juzi) usiku. Waliponifahamisha… siwezi kuelezea namna ninavyojisikia. Ninafuraha sana kuwapo hapa.


"Inamaana kubwa kwangu kwa sababu, kama nilivyosema, hii ni klabu kubwa. Msimu uliopita ulikuwa mzuri, na bila ya shaka utajirudia tena mwaka huu; pia kuna ubingwa wa Ligi ya Klabu Bingwa. Hii ni klabu ambayo daima inapigania makombe yote. Inanifanya nijivunie na ni heshima kubwa kuwa katika klabu hii. Natumai nitaweza kuisaidia timu kutwaa idadi kubwa ya mataji."

No comments:

Post a Comment