Friday, August 10, 2012

KOCHA JUVENTUS AFUNGIWA MIEZI 10

Antonio Conte

Antonio Conte

Antonio Conte

KOCHA wa Juventus, Antonio Conte amefungiwa miezi 10 baada ya uchunguzi kuhusu tuhuma za upangaji wa matokeo katika mechi.

Mwaka jana Conte, 43, aliiongoza klabu hiyo kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Italia (Serie A) katika msimu wake wa kwanza madarakani bila ya kupoteza mechi hata moja.

Conte alituhumiwa kushindwa kuripoti upangaji wa matokeo ya mechi wa klabu yake ya zamani ya Siena katika msimu wa 2010-11.

Baada ya kuhojiwa na polisi mwezi Mei, Conte alikanusha madai hayo na kwamba amedhamiria "kuthibitisha kwa nguvu zote kwamba yeye hana hatia".

mashitaka dhidi ya Conte ya kuhusika moja kwa moja na upangaji wa matokeo yalifutwa mwezi uliopita, lakini Shirikisho la Soka la Italia (FIGC) lilisema limeridhika kwamba alikuwa akifahamu kilichokuwa kikiendelea wakati akiifundisha klabu ya Siena.

Ombi la mapatano la Conte lilikataliwa na FIGC mapema mwezi huu. Alitoa pendekezo ambalo lingemshuhudia akifungiwa kwa miezi mitatu na kulipa faini ya euro 200,000.

Shirikisho hilo sasa limethibitisha kwamba atatumikia kifungo hicho kwa miezi 10.

Polisi walisema siku za nyuma kwamba Conte anachunguzwa kwa tuhuma za rushwa mchezoni kufuatia tuhuma za uoangaji matokeo ya mechi ya Serie B baina ya Siena na Novara Aprili 2011.

Msaidizi wake wa Juve ambaye alikuwa naye Siena, Angelo Alessio, pia amefungiwa miezi nane, wakati rais wa zamani wa Lecce, Giovanni Semeraro na rais wa zamani wa Grosseto, Piero Camilli wanakabiliwa na vifungo vikubwa zaidi.

No comments:

Post a Comment