Tuesday, August 14, 2012

IVANOVIC KUTOFUNGIWA KWA 'RED CARD'

Beki Branislav Ivanovic (kulia) akilimwa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu mbaya Kolarov aliyekaa chini. Picha: REUTERS

BEKI wa Chelsea, Branislav Ivanovic ataepuka kifungo baada ya kutolewa kwa kadi nyekundu katika mechi ya Ngao ya Jamii waliyofungwa na Manchester City. 

Ilidhaniwa kwamba Ivanovic angefungiwa mechi tatu, kuanzia mechi ya Chelsea ya ufunguzi wa Ligi Kuu ya England dhidi ya Wigan Jumapili. Hata hivyo, imeonekana kwamba chama cha soka cha nchi hiyo (FA) kimebadili sheria zake baada ya tukio la Michuano ya Amsterdam 2006, wakati wachezaji wa Manchester United, Paul Scholes na Wayne Rooney walipotolewa kwa kadi nyekundu dhidi ya Porto na kujikuta wakitumikia kifungo cha kutocheza mechi tatu. 

Kutokana na madiliko ya kanuni hiyo, michuano yote isiyo ya kimashindano na ambayo ni ya kujiandaa na msimu mpya ikiwamo Ngao ya Jamii, inamaanisha kwamba Ivanovic atakuwa huru kucheza mechi hiyo ya kwanza kwenye Uwanja wa DW.

No comments:

Post a Comment