Friday, August 3, 2012

CAZORLA: MIMI NI ARSENAL RASMI

Santiago Cazorla
ARSENAL wamekamilisha usajili wa kiungo wa Hispania, Santiago Cazorla kutoka klabu ya Malaga, mchezaji huyo amesema kwenye ukurasa wake wa Twitter.

"Sasa naweza kusema mimi ni mchezaji mpya wa Arsenal," alisema kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27.

Cazorla, ambaye ameichezea timu yake ya taifa mara 47 lakini alikosa ubingwa wa Kombe la Dunia kutokana na kusumbuliwa na ngiri, aliiwezesha Malaga kufuzu kucheza Ligi ya Klabu Bingwa wakati klabu yake ya zamani ya Villarreal ilishuka daraja.

Aliitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Hispania kilichotwaa ubingwa wa Ulaya mwezi mmoja uliopita na mwaka 2008 alicheza katika michuano hiyo pia.
(AFP)

No comments:

Post a Comment