Tuesday, August 7, 2012

AZAM YAMTAMBULISHA KOCHA MSERBIA

Kocha mpya wa Azam, Boris Bunjak "Boca" akizungumza wakati wa mkutano na wanahabari jijini Dar es Salaam leo asubuhi.

AZAM FC leo imemtangaza kocha mpya raia wa Serbia, Boris Bunjak a.k.a Boca, ambaye amekuja kurithi mikoba ya Muingereza Stewart Hall ambaye amemaliza mkataba wake.

Boca ambaye amezaliwa mwaka 1954 na ana leseni ya ukocha ya UEFA, amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuifundisha Azam.



Mwenyekiti wa Azam, Said Mohammed, amesema Boca ambaye ana uzoefu wa kufundisha soka kwa miaka 22 katika klabu mbalimbali za soka za Serbia, Urusi, Ujerumani na Falme za Kiarabu pia aliwahi kuwa Mkufunzi katika Chama cha Soka cha Yugoslavia.

Mserbia huyo anaendeleza tabia mpya ya klabu za Tanzania kupenda makocha Waserbia tangu, Sredjovic Milutin 'Micho', Dusan Kondic, Kostadin Papic waliopita Yanga na Milovan Cirkovic wa Simba. WASIFU KAMILI BORIS BUNJAK 'BOCA'
Boris Bunjak
Taarifa binafsi
Jina kamili Boris Bunjak
Tarehe ya kuzaliwa Novemba 17, 1954 (umri 57)
Taarifa za klabu
Klabu yake ya mwisho Al Oruba Sur
Klabu aliyocheza*
Miaka Timu Mechi (magoli)

FK Borac Cacak

Timu alizofundisha
1990-1993 FK Sloga Kraljevo )
1995-1996 FK Javor Ivanjica
1996-1997 Crvena Zvezda Gnjilane
1999 FK Radnicki Nis
2000 FC Uralan Elista
2000-2002 FK Mladi Radnik
2002-2004 FK Crvena Zvezda Beograd
2004 Al-Shaab
2005 FK Hajduk Kula
2006-2007 Al-Nasr
2009- Al Oruba Sur

No comments:

Post a Comment