Monday, August 6, 2012

BARCELONA WAMTEMA STRAIKA CHRISTIAN TELLO


Christian Tello akishangilia baada ya kuifungia klabu Barca wakati wa mechi yao ya hatua ya 16-Bora ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Bayern 04 Leverkusen kwenye Uwanja wa Camp Nou,Machi 7, 2012.
BARCELONA, Hispania
YOSSO Christian Tello hajapewa nafasi katika kikosi cha kwanza cha Barcelona kilichotolewa leo ikiwa ni wiki chache tu kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa La Liga, Ligi Kuu ya Hispania.

Straika huyo wa zamani wa klabu ya Espanyol alichezeshwa sana katika kikosi cha Barca kuelekea mwishoni mwa msimu uliopita, akishuka dimbani mara 22 katika michuano yote kuanzia Januari hadi Mei -- mwishoni mwa msimu wa 2011-12.

Licha ya kujumuishwa zaidi kikosini msimu uliopita, yosso huyo bado hajapewa namba katika kikosi cha kwanza  kinachojiandaa kwa msimu mpya, na hayumo pia katika wasifu wa kikosi cha kwanza cha timu hiyo uliomo katika tovuti rasmi ya Barca.

Jordi Alba, mchezaji pekee hadi sasa aliyenunuliwa na klabu hiyo katika dirisha la usajili wa majira ya kiangazi, amepewa jezi Na.18, sawa na aliyokuwa akiivaa wakati akiichezea timu ya taifa ya Hispania katika fainali za Euro 2012.

Wote wawili, Alba na Tello walikuwa sehemu ya kikosi cha kocha Luis Milla kilichoshiriki michezo ya Olimpiki na kutolewa mapema katika hatua ya makundi kufuatia kipigo cha kushangaza cha wiki iliyopita dhidi ya Honduras.

Barcelona watacheza mechi yao ya kwanza ya La Liga Agosti 19 dhidi ya Real Sociedad.

No comments:

Post a Comment