Friday, August 3, 2012

ARSENAL WAKOMALIA SAINI YA NURI SAHIN WA REAL


Nuri Sahin
LONDON, England
Arsenal wanaendelea kuongeza nguvu zao katika kukamilisha usajili wa kiungo Nuri Sahin anayekabiliwa na ushindani mkali wa namba katika klabu yake ya sasa ya Real Madrid.

Gazeti la The Mirror limesema leo kuwa Arsenal wako katika hatua nzuri ya mazungumzo na Real Madrid kuhusiana na mpango wao wa kumsajili kwa mkopo wa mrefu wa mwaka mmoja kiungo huyo wa kimataifa wa Uturuki.

Hata hivyo, imeelezwa kuwa Sahin amekuwa mgumu kuondoka Real na Tottenham pia wametangaza nia ya kupata saini yake, lakini Arsenal wanaamini kwamba wao ndio wenye nafasi kubwa ya kumpata kiungo huyo wa zamani wa Borussia Dortmund.

No comments:

Post a Comment